Halmashauri
ya manispaa ya Iringa imeshika nafasi ya tano kitaifa baada ya kufaulisha
wanafunzi waliomaliza shule za msingi kwa asilimia 82 kwa mwaka 2013.
Akizungumza
na mtandao huu wa www.matukiodaima.com
ofisini kwake Afisa Taaluma wa shule za msingi mkoani hapa Bwana Salmin Mndeme
alisema kuwa kwa mwaka 2013 jumla ya wanafunzi 2723 sawa na asilimia 82
walifaulu na kupata nafasi ya kuendelea na kidato cha kwanza katika shule
tofauti tofauti.
“mwaka
jana jumla ya wanafunzi 3352 walibahatika kufanya mitihani ya darasa la saba na
kati ya hao wavulana walikuwa 1618 na wasichana ni 1734, na waliofanya vizuri
katika mitihani yao ni wavulana 1317 na wasichana 1406 jumla wanafunzi wote
waliofaulu ni 2723 sawa na asilimia 82 na kwa upande wa walioshindwa wavulana
ni 286 na wasichana 314 jumla wote ni 600”. Alisema bwana Mndeme.
Hata
hivyo alisema wanafunzi hao wote walitoka katika shule 47 zilizopo manispaa ya Iringa
huku shule 41 zikiwa za Serikali na shule 6 zikiwa za binafsi na kati ya hizo
shule 40 zilikuwa zinafundisha mchepuo wa Kiswahili na shule 7 zilikuwa
zinafundisha katika mchepuo wa kiingereza.
“wanafunzi
wote
waliofaulu wameendelea na shule za sekondari ambapo jumla ya wanafunzi 6
yaani wasichana watatu na wavulana watatu walienda
shule ya vipaji maalumu na kwa upande wa shule za ufundi walienda
wavulana 6 na
msichana mmoja jumla walienda saba.” Alisema.
Pia
alizitaja shule zilizoshika tatu bora mkoani hapa ni ya kwanza ni shule ya
msingi Sipto, ya pili ni shule ya msingi Umsalama na nafasi ya tatu ilishikwa
na shule ya msingi Ukombozi.
NA
DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni