HOPE SERVICE STATION

nsekwa

ALTEZA

Jumapili, 25 Mei 2014

CHADEMA IRINGA MJINI WATIMULIWA KATIKA MAZISHI YA DEREVA BODA BODA , WASEMA WAO SI CHAMA CHA SIASA

Waombolezaji wakitoa heshima  zao huku wengine wakichukua picha za kumbukumbu 
Mhubiri aliyejitolea baada ya kanisa la Rc kususa kuendesha misa
Marehemu enzi za uhai wake 
Kijana wa boda boda akifurahia  kuwapokonya chepe wenzake 
Vijana wakizichapa ngumi kugombea kuzika 
Mwenyeji walikuwa watazamaji baada ya boda boda kuchukua jukumu zima la kuzika katikati ni mwenyekiti wa waganga wa tiba asilia mkoa wa Iringa Galusi Msekwa 
Dereva wa bajaji iliyobeba mwili wa marehemu 
Kijana aliyejitolea kuendesha ibada ya mazishi kulia akisaidiana na ndugu kuweka msalaba 
Mwakilishi wa kundi la Mundu Sanaa Group Bw Lackson akiweka shada la maua 
Mwenyekiti wa chama cha boda boda Iringa Joseph Mwambope akiweka shada la maua 
Huyu ndie kada wa Chadema aliyepewa nafasi ya kuweka shada na kuambilia kuzomewa 

Mwenyekiti wa chama cha boda boda na Bajaji Iringa Joseph Mwambope akizungumza katika mazishi hayo
............................................
Na www.mwandishiwetu.blogspot.com
MATUMAINI ya vijana dhidi ya chama   demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Iringa mjini   imeanza kutoweka baada ya jana dereva  boda boda zaidi ya  200   kuwazuia  viongozi wa Chadema kupeperusha wala kufunika bendera  za chama  hicho katika bajaji iliyobeba mwili wa dereva mwenzao Abisai Mdesa .

Vuta nikuvute hiyo  ilitokea majira ya saa 4 asubuhi  baada ya  makada wa Chadema  kufika Chumba cha maiti  katika  Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa  wakiwa na bendera za Chadema kwa ajili ya kuwapa  madereva  wa boda boda pamoja na kufunga katika bajaji iliyopaswa  kubeba mwili wa marehemu huyo bado bado msimamo wa  boda bado ulionekana kupingana na matakwa ya  viongozi hao.

Vijana  hao  walionesha  kupinga msimamo wa makada hao wa Chadema kutoka  kufunika bendera wa chama chao katika jeneza la marehemu huyo  wala kupeperusha bendera ya chama chao katika msafara wa mazishi kwa madai kuwa chama hicho cha boda boda Iringa si chama cha kisiasa na wala hakina ubia na Chadema .

Wakizungumza kwa jazba  vijana  hao  waendesha  boda  boda boda  walisema  kuwa  wamesikitishwa na kitendo cha Chadema kutaka kujipatia umaarufu kupitia mazishi ya dereva mwenzao  huyu hali  wakitambua kuwa  wao  si sehemu ya Chadema.

Walisema walikuwa tayari  kuwashambulia kwa  kipigo makada hao wanne wa Chadema  waliofika na bendera  hizo iwapo  wangeshindwa kuwasikiliza na kuendelea na msimamo wao wa  kufunga bendera.

Mwenyekiti wa chama  cha  boda boda na Bajaji mjini Iringa Joseph Mwambope  aliwaeleza  waandishi wa habari kuwa  hatua ya Chadema  kutaka  kujimilikisha msiba  huo ni kosa kubwa na kuwa wanachotambua kuwa  marehemu hakuwa kiongozi wa Chadema ila alikuwa ni mwanachama wa chama cha boda boda hivyo mbali ya ndugu mwenye nafasi ya  kuendesha mazishi hayo ni  chama  cha boda boda na Bajaji pamoja na wasanii wenzake wa Mundu Sanaa Group na sio chama  chochote cha siasa.

"Tunaomba ieleweke  kuwa chama cha boda boda si  chama  cha kisiasa  hivyo haturuhusu Chadema ama CCM kuja na bendera za  vyama  vyao katika msiba  huu japo hatuwakatazi  kuja na magari  yao yakiwa na bendera  za  vyama  vyao ila sio kuleta bendera tufungi kwenye boda boda na bajaji zetu "alisema Mwambope

Kuwa  imekuwa ni kawaida ya Chadema na  vyama vingine  kujipendekeza katika misiba ambayo wanahisi ina waombolezaji  wengi ili  kutumia nafasi hiyo kujitangaza kisiasa ila  wakati wa  kuuguza vyama  hivyo huwa havitokei kuuguza.

" Huyu mwenzetu mbali ya kupata ajali ya  pikipiki kwa siku zaidi ya nne  sasa alikuwa amelezwa  Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na madereva tulianza kuchangishana  ili kumfanyia rufaa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili .....sasa kama Chadema ambao  leo wanakuja na bendera wapo kwanini  wasingetoa usafiri wa kwenda Muhimbili kama si kutaka kuonekana sasa baada ya kifo"

Katika hatua  nyingine vijana  hao wa boda boda  walilazimika  kuzomea kada wa Chadema aliyepewa  kuweka shada kaburini kutokana na kushindwa kukabidhi ahadi yao ya mchango wa shilingi 25000 ambazo waliahidi kwenye daftari la waombolezaji bila kutoa pesa  hiyo .

Kijana   huyo  enzi  za uhai  wake  alikuwa ni mpenzi wa Chadema ambae mara kadhaa alionekana kupanda juu ya miti mirefu na kufunga bendera  za Chadema .
MWISHO 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni