Madereva
wa mkoani Iringa wanaoendesha magari ya kubebea watu almaharufu kama daladala wamefanya
mgomo wa kutopakia abiria kwa kile kinachosemekana kuwa wananyanyaswa na askari
walioko barabarani.
Akizungumza
na mtandao huu wa www.matukiodaima.com
mmoja wa madereva hao bwana Bisheni Mgwilanga alisema kuwa trafki wanataka gari
ipakie levo siti na hakuna mtu au abiria kusimama kitu ambacho hakiwezekani kwa
wao na hata abiria pia.
“lengo
la kurundika magari hapa sisi kama sisi tunalilia haki kwa hawa askari wanaolinda
usalama barabarani wanatunyanyasa sana wao
wanatuambia tupakie levo siti na ukiangalia tajiri anataka elfu sabini mafuta
tujaze ya elfu tisini na rooti tunazokaa kituoni tunaenda mara tatu kwa siku
kiasi kwamba huwezi kupata hata laki moja na thelathini hapo unategemea bosi
utampelekea nini?,
ukijaza gari kiasi cha kawaida tu ukifika hapa
wanaposimamaga maeneo ya darajani wanatusimamisha wanatuambia tumejaza sana na
wanachukua elfu thelathini inabaki laki moja tajiri unampa 70 yake inabaki 30
hapo mafuta bado mimi sijapata ela ya kuacha mezani watu tuna wake na watoto
sasa tumechoka tunataka haki hapa, tunahitaji watuitie RTO tuongee nae” alisema
bwana Mgwilanga.
Mtandao
huu haukuishia kwa madereva tu ukapanda mpaka kwa Sumatra na kutaka kujua ni
taratibu gani gari aina ya daladala inayofanya mizunguko yake maeneo ya hapa
karibu na upoje katika kubeba abiria? Tulipofika ofisi za Sumatra tulikutana na
Afisa mfawizi wa Sumatra bwana Rahim Kondo ambapo alisema kuwa hakuna gari
inayofanya kazi maeneo ya karibu na mjini ambayo haikuruhusiwa kusimamisha
abiria bali dereva anaruhusiwa kupakia abiria wanaoweza kukaa katika hilo gari na
mlango ukafungwa vizuri pindi wanapoianza safari yao.
“
tukisema magari yapakie levo siti itakuwa ni balaa maana abiria hawatoisha
mjini kwani wapo wengi sana ila tulichowaambia wapakie abiria wanaoweza
kuwabeba na wahakikishe milango ya magari yao inafungwa hapo sisi hatutakuwa na
kesi yeyote kwa dereva kama akifanya hivyo, amepakia abiria wake na mlango
kaufunga wala haina shida kwani daladala zetu zinatembea kituo hiki na hiki
kasimama anashusha abiria wake basi
anaendelea na safari yake tofauti na magari yanayoenda umbali mrefu wao
haturuhusu kusimamisha abiria hata siku moja kwani tunaogopa ajali
zisizotarajiwa” alisema bwana Kondo.
Hata
hivyo alisema endapo kama kuna dereva atapakia abiria mpaka mlangoni na
kushindwa kufunga mlango basi akikamatwa ni haki yake maana kakiuka masharti
yaliyoandikwa katika leseni aliyopewa na Sumatra.
Mpaka
inafika jioni bado magari yaendayo maeneo ya Cagrielo, Kiwandani na Igumbiro
hayakurudi kazini na kwa upande wa magari yaendayo Kihesa, Tumaini, Mkimbizi na
kwingineko yao yalianza mgomo mida ya alasiri baada ya viongozi wao bwana
Walter ambaye ni kiongozi wa magari yaendayo cagrielo, kiwandani na igumbiro
pamoja na bwana best kiongozi wa magari yaendayo kihesa, tumaini na mkimbizi
kushikiliwa na polisi kwa muda lakini waliachiwa na magari yakarudi kazini kama
kawaida.
NA
DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni