Peter Muthirika anayeongoza chama cha DPP ndiye rais mteule nchini Malawi
.............................................................................
Hatimaye Malawi imepata Rais mpya baada ya mivutano ya kisheria kwa wiki nzima.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amesema kutoka
mjini Blantyre kuwa Profesa Peter Mutharika ameshinda uchaguzi huo kwa
kupata asilimia 36.4 ya kura zote akifuatiwa na Dr Lazarus Chakwera
mwenye asilimia 27.8 huku Rais anayemaliza muda wake Dr Joyce Banda
akishika nafasi ya tatu kwa asilimia 20.2 na Atupele Muluzi amekuwa wa
nne na asilimia 13.7
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji
Mackson Mbendera amesema uchaguzi huo ulikumbwa na changamoto nyingi
lakini mwishowe nchi ni lazima ipate kiongozi wake na kuwaomba wananchi
kuwa na utulivu .
Kesi Mahakamani
Awali Jaji Kenyata Nyirenda wa mahakama kuu
mjini humo jana usiku alitoa uamuzi kuwa hawezi kuvunja sheria kwa
kuruhusu tume iongeze muda wa kuhesabu upya kura kwenye maeneo yenye
utata.
Na kwamba sheria inaitaka tume kutangaza matokeo ndani ya siku nane na si vinginevyo.
Uchaguzi wa Malawi ulifanyika Mei 20 nchini kote
lakini siku moja tu baada ya kupiga kura, malalamiko yakiambatana na
mapingamizi ya kisheria yakatawala kwenye mahakama kuu za Lilongwe na
Blantyre.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni