Amesema Rais hana mamlaka ya kuingilia tume ya uchaguzi ambayo inafanya kazi kikatiba na kisheria. Pia Rais Wa chama cha wanasheria wa Malawi (MLS) na Pia Mwanasheria Mkuu wa Zamani wa Malawi wameongea na Vyombo vya Habari Mud Mfupi uliopita na kusema ibara aliyoitaja Rais haimpi mamlaka ya kufuta uchaguzi..
Wamesema kifungu cha 5 cha sheria ya uchaguzi wa Bunge na Rais kinaipa Mamlaka Jukumu lote tume ya uchaguzi kusimamia mchakato wa Uchaguzi. Pia kifungu cha 100 cha sheria hiyo kinatoa haki ya chama au mgombea kulalamika kwa tume kuhusu ukiukwaji wa Mwenendo wa Uchaguzi na kama ndani ya masaa 48 hali hiyo isiporekebishwa kwa kiwango cha kuridhishwa basi kifungu namba 113 cha sheria hiyo hiyo kitatumika kupeleka mashtaka Mahakama Kuu.Hata hivyo Mwanasheria mkuu akizungumzia Amri hiyo ya Rais leo hii amesema "Kuna Mtu anafanya uhaini hapa sasa" na kuendelea kudai kuwa Rais amefanya uhaini kwa kukiuka ibara ya 88 ya katiba ya nchi kutoa "Presidential Decree" bila sababu yoyote ya msingi inayozingatia katiba na mamlaka ya kisheria
Rais Joyce Banda muda mfupi uliopita ameatoa Amri kwa Tume ya Uchaguzi ya Malawi(MEC) Kuacha mara moja kutangaza matokeo na kufuta uchaguzi ambao vyama viwili vya Upinzani vilikua vikiongoza.Ametaka uchaguzi uitishwe kwa kipindi cha Siku 90 zijazo
Chama cha Wanasheria Malawi nacho kimesema Rais hana Mamlaka ya kisheria/kikatiba kusitisha mchakato wa kutangaza Matokeo ya uchaguzi
Kama nilivotabiri tangu juzi kuwa kuna kila Dalili ya Mama huyu kutia Aibu nyingine kwa Taifa lake na Afrika Kwa Ujumla
-Alipoona Peter Mutharika anaongoza alituma jeshi na pia polisi nyumbani kwake
-Naibu waziri wake aliposhindwa Ubunge alijipiga risasi na kujiua
-Chama chake kilivituhumu vyombo vya habari kwa kupendelea upinzani
-Jana alipeleka Pingamizi mahakamani kuzuia matokeo kutangazwa na kukituhumu chama cha upinzani kufanya wizi wa kura.Mahakama ilitupilia mbali pingamizi hilo kwa hoja kuwa halina msingi
-Jana hiyo hiyo mkuu wa idara ya habari na Matangazo alifukuzwa kazi kwa kukiuka Amri ya Serikali ya kusitisha matangazo ya matokeo ya uchaguzi.Chama cha Wanasheria Malawi kikasema kuwa kilichofanyika ni uonevu mkubwa.
Hawa ndio madikteta wa Afrika wasiotaka kushindwa uchaguzi
Roodney alipoandika "People's Power ,No Dictator" alisema kuwa "Madikteta wanajikweza na pia kuinuliwa na watu.Wanajiona wako juu ya Watu,Taasisi na oganization Zote.Wanainuliwa na kutukuzwa na watu,taasisi,viongozi wa Dini na viongozi wa Kimila".Hii ndio picha halisi ya viongozi wa Afrika
Sasa anachotafuta Joyce Banda ni Vurugu ili atangaze hali ya Hatari na afanye Suspension ya Katiba in order to assume fully dictatorial power.
Jumuiya ya Kimataifa hasa SADC,COMESA,AU na UN hazitakiwi kuruhusu hali iliyojitokeza Nigeria Mwaka 1993 ya Dikteta Ibrahim Babangida kufanya nullification ya Matokeo ya Urais yaliyokua yamempa Ushindi Chifu Mashoud Abiola na baadae Abiola kuwekwa ndani akiwa President Elect hadi miaka 5 ilipopita na kufanyiwa hujuma akiwa Gereni pia chini ya Utawala wa Mtawala wa kijeshi Dikteta Sani Abacha. Chifu Abiola alikufa kifo cha Kutatanisha baadae kabla Olusegun Obasanjo hajaachiwa Kutoka Gerezani na kuongoza mageuzi ya kisiasa kwa msaada wa jumuiya ya kimataifa baada pia ya kifo cha ghafla cha dikteta Sani Abacha.
We must cherish the values of Democracy.Kama AU inakata Mapinduzi (Coup d'etat) dhidi ya Tawala zilizochaguliwa Kidemokrasia,kwanini turuhusu watawala kupindua matakwa ya umma kupitia sanduku la kura(Coup d'Civillien)?
Hili halitakiwi kuachwa hata kidogo karne hii
Upinzani Tanzania tujiandae kukabiliana na hali hii Mwakani.Naamini Upinzani Malawi Utasimama kidete bila kuyumba kukabiliana na udikteta huu.Tume ya Uchaguzi ya Malawi hadi sasa imeonyesha Msimamo bila woga.
Matokeo ya Urais Malawi hadi jana jioni yalikuwa hivi:,
1:Prof.Peter Mutharika wa DPP 1,789,364 ,
2:Lazarus Chakwera wa MCP 1,388,500,
3:Joyce Banda wa PP 1,042,686,
4:Atupele Muluzi wa UDF 665,519
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni