TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Kufutia kuibuka kwa vikundi vya
vijana vinavyojulikana kwa majina ya mbwa mwitu, watoto wa mbwa au Panya
road na kujihusisha na vitendo vya kihalifu ikiwemo uporaji,
unyang’anyi wa kutumia nguvu na kujeruhi watu katika maeneo mbalimbali
jijini Dar es salaam, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (DIGP)
Abdulrahaman Kaniki amewaagiza makamanda hususani wa Kanda Maalumu ya
Dar es salaam kuhakikisha wanavitafuta vikundi hivyo popote vilipo,
kuwakamata na kuwafisha katika vyombo vya sheria.
Naibu IGP amekemea vikali vikundi
hivyo na kuvitaka kuacha tabia hiyo mara moja, kwani vitendo hivyo ni
vya kihalifu na vinatakiwa kukemewa na kila mtu katika jamii.
Aidha, amewataka wananchi kuondoa
hofu na badala yake watoe ushirikiano kwa kutoa taarifa za vikundi hivyo
katika vituo vya Polisi ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni