Taifa
Stars na Malawi (Flames) zinapambana Jumanne (Mei 27 mwaka huu) katika mchezo
wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 11
jioni.
Mechi
hiyo itakuwa ya mwisho kwa Taifa Stars kujipima kabla ya kucheza mchezo wa
marudiano wa michuano ya Afrika na Zimbabwe (Mighty Warriors) utakaofanyika
Juni Mosi mwaka huu jijini Harare.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini Tukuyu mkoani Mbeya chini
ya Kocha wake Mart Nooij kujiandaa kwa mechi dhidi ya Malawi na ile ya
Zimbabwe.
Malawi
imewasili leo mchana (Mei 24 mwaka huu) kwa ndege ya Malawian Airlines kwa
ajili ya mchezo huo ikiwa na msafara wa watu 27, na imefikia kwenye hoteli ya Sapphire
Court iliyopo Mtaa wa Lindi jijini Dar es Salaam.
Flames
inayofundishwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Malawi, Young Chidmozi
inatarajia kufanya mazoezi leo jioni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Baada
ya mechi hiyo, Malawi itakwenda moja kwa moja nchini Chad kwa ajili ya mechi ya
marudiano ya michuano ya Afrika itakayochezwa Mei 30 mwaka huu jijini Ndjamena.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni