Tanzania
inaendelea kufanya vizuri kwenye Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) kwa upande
wa mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 baada ya leo (Mei 23
mwaka huu) baada ya kuwachapa wenyeji Botswana mabao 2-0.
Mabao
ya Tanzania katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa SSKB jijini Gaborone
yalifungwa na David Uromi dakika ya sita huku Anthony Amede akitupia la pili
dakika ya 46.
Katika
mechi yake ya kwanza, Tanzania ilitoka sare ya bao 1-1 na Mali ambapo michezo
hiyo inaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha SuperSport cha
Afrika Kusini.
Tanzania
itacheza mechi yake ya tatu keshokutwa (Mei 25 mwaka huu) dhidi ya Swaziland,
itakuwa tena uwanjani Mei 27 mwaka huu kuikabili Nigeria wakati mechi ya mwisho
itafanyika Mei 29 mwaka huu dhidi ya Afrika Kusini.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni