Mwili wa marehemu Geofrey Mlelwa (26) ukiwa katika gari la polisi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa leo |
Baba mzazi wa kijana Mlelwa mzee Guriano Mlelwa kulia mwenye kofia akitazama gari hilo la polisi lenye mwili wa kijana wake |
Baba mzazi wa kijana Mlelwa mzee Guriano Mlelwa kulia mwenye kofia akitazama gari hilo la polisi lenye mwili wa kijana wake |
Gari la polisi likiwa na mwili wa kijana huyo |
MBALI ya jitihada mbali mbali zinazofanywa na makampuni ya kutengeneza pombe kutoa tahadhari katika chupa za pombe hizo kuwa unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako ila bado baadhi ya watu wameendelea kupuuza tahadhari hizo na kuendeleza tabia ya kunywa pombe kupita kupindukia kiasi cha kusababisha kuhatarisha maisha kama kijana mkazi wa Ipogolo mjini Iringa Geofrey Mlelwa (26) aliyeamua kukatisha maisha yake kwa unywaji pombe.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia leo jumatatu katika eneo la Ipogolo mjini hapa ambapo kijana huyo kuli katika soko kuu wa Manispaa ya Iringa akiwa na wenzake alipoamua kuuchapa ulabu kiasi cha kushindwa kujitambua na kupelekea kifo chake.
Wakizungunza na mwandishi wa habari hizi baadhi ya mashuhuda walisema kuwa kijana huyo enzi za uhai wake alikuwa ni mtu wa kunywa pombe za kienyeji aina ya ulanzi na bangi ila siku hiyo ya tukio alionekana ni mwenye pesa hivyo kuachana na kunywa pombe aliyoizoea na kuanza kunywa pombe ya kisasa kwa kuchanganya Grant na viroba na ulanzi ndani ya chupa mmoja.
Hata hivyo walisema sanjari na kumshauri kutumia pombe ambayo aliizoea ila bado aliendelea kupuuza na kutumia pombe hiyo mpya kwake kwa kunywa kupita kiasi.
Mbali ya kunywa pombe hiyo ila kijana huyo hakuweza kula chakula chochote toka alipoanza kunywa pombe hiyo na alipozidiwa rafiki yake alimkokota na kumpeleka chumbani kwao (getho) kabla ya asubuhi kuamka na kumkuta amekufa .
Baba mzazi wa kijana huyo mzee Guriano Mlelwa allithibitisha kutokea kwa kifo cha kijana wake na kuwa chanzo cha kifo hicho ni unywaji wa pombe kupita kiasi .
Alisema kuwa kwa kawaida kijana wake anamtambua kama ni mlevi wa pombe na mtumiaji wa madawa ya kulevya na kuwa hata katika chumba chake walimkutana na chupa ya pombe aina ya grant ambayo ndani yake ilikuwa imechanganywa pombe mbali mbali pamoja na viroba (konyagi).
Hivyo alisema anaamini kuwa mchanganyiko huo wa pombe na matumizi ya dawa za kulevya ndio umesababisha kifo hicho hivyo kuwashauri vijana kuachana na matumizi ya pombe kupita kiasi na madawa ya kulevya kwani wakiendelea kilichomuua mwenzao ndicho kitakachowaua pia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni