WANANCHI
wa kijiji cha Ibumu katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
wamewatuhumu viongozi wao wa serikali ya kijiji hicho kuwa ni
vinara wa ulimaji katika vyanzo vya maji .
Wakizungumza
katika mdahalo wa usimamizi shirikishi wa raslimali maji ,misitu na
fedha za umma ulioandiliwa na asasi ya kiraia ya MMADEA juzi
wananchi hao walisema kuwa sehemu kubwa ya wananchi wa kijiji
hicho wanaendesha maisha yao kupitia kilimo cha maeneo yenye maji
maarufu kama vinyungu wakiwemo viongozi wa serikali ya kijiji hicho.
Hivyo
kitendo cha asasi ya MMADEA kufika kijijini hapo kwa ajili ya kuunda
mtandao wa kusimamia rasilimali hizo ikiwemo ya maji na misitu
viongozi hao waliona ni kama mwiba kwao kutokana na kuwa wao
wenyewe ndio wanaoongoza kwa uharibifu wa mazingira katika maeneo
ya vyanzo vya maji.
Wananchi
hao
waliomba MMADEA kwa kushirikiana na serikali ngazi ya wilaya kuweka
mkakati wa pamoja na kulinda vyanzo vya maji kwa faida ya vizazi
vijavyo badala ya kuendelea kuwafumbia macho viongozi wa serikali
ambao hawapo tayari kulinda vyanzo hivyo vya maji.
Mbali
ya kuwataka viongozi hao kubanwa kwa kushindwa kulinda vyanzo
vya maji bado wananchi hao walisema kumekuwepo na usimamizi mbaya
wa fedha za
umma zinazotolewa katika kijiji hicho kwa ajili ya shughuli na
maendeleo .
"
Tunashangazwa sana na viongozi wetu wa serikali kushindwa
kushirikia nasi katika mdahalo huu na kukimbia wakati lengo la MMADEA
ni kwa faida yetu wenyewe .......sasa tunaomba hatua zichukuliwe
kwa viongozi wetu ambao watabainika kuwa sehemu ya uharibifu wa
mazingira katika vyanzo vya maji "
Hata
hivyo vingozi hao mwenyekiti na mtendaji wa kijiji hawakuweza
kupatikana kuzungumzia tuhuma hizo dhidi yao huku mmoja kati ya
wajumbe wa serikali ya kijiji hicho ambao aliomba jina lake
kuhifadhiwa kwa kuwa si msemaji wa serikali ya kijiji hicho
,alisema kuwa mwenyekiti wa kijiji na mtendaji pamoja na diwani wao
ni miongoni mwa wananchi wanaolima katika vyanzo vya maji na ndio
sababu ya kushindwa kufika katika
mdahalo huo.
Pia
alisema viongozi hao ndio waliopanga vijana kuvuruga mdahalo huo
uli usifanikiwe kama njia ya kuficha suala hilo la wao kulima
katika vyanazo vya maji.
Mkuu
wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita alisema kuwa zipo sheria
zinazoelekea mita za kulima kutoka katika vyanzo vya maji na kuwa
serikali ya wilaya hiyo haitakuwa tayari kuona wananchi wakilima
katika vyanzo vya maji na hivyo kuwataka viongozi na wananchi
wanaoendelea kulima katika vyanzo hivyo kuondoka wenyewe kabla ya
kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Mratibu wa MMADEA
mkoa wa Iringa Raphael Mtitu alisema kuwa mdahalo huo ulilenga
kuwaelimisha wananchi ili kuweza kushiriki katika uhifadhi wa misitu
na maji katika maeneo yao .
Alisema
kuwa asasi hiyo imekuwa ikifanya kazi katika tarafa ya Mahenge na
Mazombe katika wilaya ya Kilolo pia alisema faida kubwa ya
uhifadhi wa mazingira ni pamoja na wananchi hao kupata mvua ya
kutosha na
kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yameendelea
kulikumba Taifa na dunia kwa ujumla .
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni