Washiriki wa Redd's Miss Iringa 2013 WAKATI shindano la kumsaka mrembo wa Redd's Miss Iringa 2014 limepangwa kufanyika Juni 6 mwaka huu hadi sasa maandalizi yako mkoani Iringa hayaeleweki na ukimya umeendelea kutanda . Baadhi ya warembo ambao walipanga kujitosa katika ulingo huo wameonyesha kukata tamaana ya kushiriki kwao huku baadhi yao wakijiandaa kwenda mikoa ya jirani kutimiza azma yao. Wakizungumza na mtandao huu wa www.mwandishiwetu.blogspot.com baadhi ya warembo hao kutoka chuo cha Iringa , Ruco na Mkwawa ambao walijipanga kujitosa katika ulingo wamedai wamevunjika moyo na maandalizi ya zoezi hilo na hivyo kuamua kuahirisha kujitosa . Kwani walisema kwa miaka mingine zoezi hilo huwa linafanyika katika hali ya uwazi mkubwa na maandalizi yake huwa yanaanza mapema ila kwa mwaka huu hakuna kinachoendelea huku siku zikizidi kuyoyoma. Alisema mrembo Amina kuwa kuna uwezekano mkubwa wa shindano hilo kwa mwaka huu likakosa mvuto na hata mrembo atakayepatikana kutouzika katika mashindano ya kanda kutokana na maandalizi ya kiubabaishaji ambayo yanaendelea kimya kimya. " Tunashangaa sana miaka mingine hadi sasa fomu kwa washiriki zinakuwa zimetolewa na kambi limeanza ila mwaka huu japo kusikia kuwa kambi lingeanza toka May 22 ila hadi leo ni may 26 ila hakuna kinachoendelea.....sasa kuna maandalizi hapo ama ubabaishaji" Hata hivyo walimtaka muandaaji wa shindano hilo kwa mwaka huu kuiga mfano wa muandaaji wa mashindano kama hayo mkoa wa Tanga ambapo anatoa gari kwa mshiriki wa shindano hilo. Jitihada za mtandao huu kumtafuta mratibu wa shindano hilo zinaendelea ili kuweleza sababu za kuchelewa kuanza maandalizi hayo |
HOPE SERVICE STATION
nsekwa
ALTEZA
Jumatatu, 26 Mei 2014
WAREMBO IRINGA WASHITUKIA SHINDANO LA REDD's MISS IRINGA 2014
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni