NAIBU katibu mkuu wa
chama cha mapinduzi (CCM) Bara Mwigulu Nchemba awahakikishia wananchi wa jimbo la Iringa mjini kuwa muda wa mbunge wa jimbo hilo kuongoza umefika kikomo na kuwa
ataongoza mapambano ya kumng’oa mwakani katika uchaguzi mkuu.
Akiwahutubia
wananchi wa jimbo la Iringa mjini
leo katika uwanja wa Mwembetogwa Nchemba ambae ni naibu waziri wa fedha alisema kuwa mbali ya mbunge huyo kupewa nafasi hiyo ya bure mwaka 2010
ila bado ameshindwa kuwa na huruma na
wananchi wa jimbo hilo na kuendelea
kujinufaisha yeye badala ya kuwekeza kwa
wananchi hasa vijana na ndio sababu ya kushindwa kufanya vikao na
wanachama wake na kuendelea kuitisha maandamano badala ya kufanya kazi.
“Tutajipanga vema
kila kona ya jimbo la Iringa mjini ili kulirudisha jimbo mikononi mwa CCM
kwa kumpata mbunge ambae atawatumikia
wananchi na sio wa kujitumikia yeye na kuwa mbunge wa maandamano kwa
kipindi chake chote”
Nchemba alisema kuwa kutokana na kazi kubwa iliyopfanywa na vijana wa jimbo la
Iringa kwa kumpigania mbunge Msigwa alipaswa
kuwa na roho ya huruma kwa vijana hao ikiwa ni pamoja na kuwageuza
daraja na kuwafanyisha maandamano yasiyo kwisha badala ya kuwaanzishia miradi
ya kiuchumi.
“Hivi tazameni leo maeneo
yote ya makanda wa Chadema majimboni mwao ni maandamano kila siku kila
wakati utasikia hakuna kulala makamanda huku mbunge anashindwa kuwasaidia …..na
siku hizi wanakuja na hoja ya makamanda
pambaneni tutachukua nchi huku hata kata kwao ni ndoto sasa niwaambie leo hata nusu ya nchi hii kamwe hawatapata”
Asema mmoja kati ya
mke wa kiongozi mojawapo wa Chadema
alimuuliza hivi kwa nini mume wake anapenda
sana maandamano alimjibu kuwa
mume wake huyo akichukia huwa anafanya maandamano ndani
ya chumba cha kulala.
Nchemba pia
ameponmgeza utendaji kazi wa mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta
Kabati na kuwa siku zote
amekuwa akiwapigania wananchi wa jimbo la Iringa mjini bungeni tofauti
na mbunge wa jimbo mchungaji Msigwa ambae amekuwa akiongoza kwa kufanya
maandamano.
Katika hatua nyingine
Nchemba alisema amesema kuwa muda wa
matajiri kuendelea kujinufaisha na
misamaha ya kodi umekwisha na kuwa anajipanga kupeleka muswada bungeni ili kutungwa sheria itakayowabana
wafanyabiashara wakubwa kulipa kodi kama
wanavyolipa wafanyabiashara
wadogo.
Alisema kuwa
watu wanapata misamaha hadi inakatisha tamaa kwani ni pesa nyingi za
kimaendeleo zinapotea kutokana na
utitiri wa misamaha inayoendelea
kutolewa .
“Napeleka sheria katika bunge hili la bajeti itakayofuta misamaha ya kodi
kwa viwanda na wafanyabiashara wakubwa…inakuweje wananchi masikiti hata wanapotaka kuanzisha saluni wanalipizwa kodi ila
wafanyabiashara wakubwa na baadhi
ya watu pia nitapeleka sheria ya kubana
matumizi ya fedha za umma”
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni