Aliekuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Njombe, Adam
Ismail Msigwa (pichani) ambaye alijukana kwa jina maarufu kama
'Shilingi ni Vita' amefariki jana usiku wa kuamkia leo nyumbani katika
Mitaa wa Kwivaha Njombe mjini na mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho
kijijini kwake Lusitu.
Marehemu Adam Msigwa ambaye ni baba
mlezi wa mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Iringa, Jesca Msavatavangu ambaye
ni mjombe wake na Spika wa Bunge, Anna Makinda amefarika dunia jana
usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua ghafla kwa ugonjwa wa shinikizo la
damu (BP) pamoja na matatizo ya moyo. (NA FRIDAY SIMBAYA, NJOMBE)
Mwenyekiti wa Wilaya ya Njombe mjini, Adam Msigwa (mwenye kofia) enzi za uhai wake akiwa na Mkuu wa Wilaya Njombe Sarah Dumba wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2011.
Marehemu Adam Msigwa (kulia) akiwa na Bazili Mramba enzi za uhai wake.
Mkuu wa
Mkoa wa Njombe Capt. Aseri Msangi (wa pili kushoto) akibadilishana
mawazo na mdogo wa marehem, Abubakari Msigwa (wa mwisho kulia)
walipofika nyumbani kwa marehemu leo asubuhi.
Marehemu Adam Isimail Msigwa (kulia) akisalimia na Rais mstaafu Benjamin William Mkapa mwaka 1995 enzi za uhai wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni