Suala la muungano limejaa mauzauza mengi kiasi kwamba watawala wanashindwa kujibu maswali na hoja za msingi juu ya muungano huu.
Wanacho kifanya ni kuwatishia wananchi kuwa jeshi litachukua nchi au Sultan atarudi Zanzibar. Huu ni uongo na upotoshaji mkubwa.
Hili swa la muungano wa nchi zetu mbili lina leta maswali mengi kuliko majawabu.
Hili swa la muungano wa nchi zetu mbili lina leta maswali mengi kuliko majawabu.
Nitafanya uchambuzi kidogo wa muungano wetu huu batili. Kwa kifupi nchi inayoitwa Tanzania ni batili.
Ubatili wake unakuja pale ambapo ilianzishwa na mtu moja, Nyerere, bila kushirikisha upande wa pili ( Zanzibar na Bunge laki): hata waTanganyika hawakushirikishwa.
Ubatili wake unakuja pale ambapo ilianzishwa na mtu moja, Nyerere, bila kushirikisha upande wa pili ( Zanzibar na Bunge laki): hata waTanganyika hawakushirikishwa.
Ili Muungano uwe halali kisheria, ni budi hati ya muungano iwe ratified
na Bunge la Zanzibar. Ukweli ni kuwa Bunge la Zanzibar halijawahi
kupitisha hiyo hati.
Hadi leo hiyo hati haipo kwenye hansard ya Bunge la Zanzibar, Nyerere
alitumia ubabe kuwalazimisha Zanzibar muungano; kwa kweli sijui malengo
yake yalikuwa ni nini.?
Ubabe huu unadhihirika pale alipo lazimika kuiuwa Tanganyika na kutunga
"decree" tatu baada ya yeye kukutana na Karume. Tunajua decree hutungwa
na nchi iliyo chukuliwa na jeshi.
Nyerere kwa ubabe wake alibadirisha mambo ya Tanganyika kuwa ya
muungano, mfano, nembo ya Tanganyika ikageuzwa ya muungano, office za
Tanganyika zika geuzwa za muungano, Katiba ya Tanganyika ikawa ya
muungano, mahakama kuu kuwa ya muungano nk.
Haya yote alifanya yeye binafsi kwa amri (decree) bila kuwashirikisha
waZanzibar (Bunge la Zanzibar) wala waTanganyika. Huu ni udicteta.
Kwa history hii kama kuna mtu atakuwa anashangaa kwa nini waZanzibar
wana chuki na Nyerere na Tanganyika; atakuwa close minded na hataki
kuukabili ukweli.
Zanzibar ni nchi ambayo ilikuwa huru kabla ya muungano na sasa imesema
haitaki huu muungano wa mauzauza. Utailazimisha muundelee kuungana nayo?
Tuwe wakweli, wapenda haki na wahalisia.
The only way tutaweza kuishi kwa amani na Ndg zetu waZanzibar ni kuipa
Zanzibar mamlaka kamili au kudisolve huu muungano batili. Serikali mbili
au moja WONT WORK.
Tatu ndio jawabuOtherwise; muungano huu batili ni time bomb ambalo lina subiri kulipuka muda wowote
Kumbukeni; Zanzibar ni nchi kamili kama Kenya na Uganda; ilipata Uhuru
wake kwa kumwaga damu, sio kama sisi tulipata kwa bwerere na ndio maana
akili zetu hazitaki kukabili ukweli.
Zanzibar ina Rais wake na Kikwete leo hii akienda Zanzibar hana sauti;
huenda kam mualikwa (mgeni). Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya muungano
Mizengwe Pinda huwa hakanyagi Zanzibar ( kuna mtu amewahi sikia Pinda
kaenda Zanzibar kusimamia miradi ya maendeleo?). Hii inazihirisha pasi
na shaka kuwa Pinda sio Waziri wa muungano, bali wa Tanganyika.
Tanganyika ipo ila watawala dharimu wa CCM wanaiogopa.
Leo hii Kikwete akienda Zanzibar hapigiwi mizinga 21; Dr. Shein ndio
anapigiwa. Sasa hapo Mkuu wa nchi ni nani? Shein au Kikwete?
Lazima kama vijana wa kizazi kipya, tujifunze kudadisi na kusaka ukweli;
sio kubuluzwa na haya MA CCM ambayo yameishiwa mbinu za kutawala na
kubaki kutumia mabavu.
TAFAKARI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni