HOPE SERVICE STATION

nsekwa

ALTEZA

Jumatatu, 26 Mei 2014

WAREMBO IRINGA WASHITUKIA SHINDANO LA REDD's MISS IRINGA 2014

Washiriki wa Redd's Miss Iringa 2013 

WAKATI  shindano la kumsaka mrembo wa Redd's Miss Iringa 2014  limepangwa kufanyika  Juni 6  mwaka huu  hadi  sasa maandalizi  yako mkoani Iringa hayaeleweki na ukimya  umeendelea  kutanda .

Baadhi ya  warembo ambao  walipanga  kujitosa katika ulingo  huo wameonyesha kukata tamaana ya kushiriki kwao huku baadhi yao  wakijiandaa kwenda mikoa ya jirani   kutimiza azma yao.

Wakizungumza na mtandao huu wa www.mwandishiwetu.blogspot.com  baadhi ya  warembo hao kutoka chuo cha Iringa , Ruco na Mkwawa ambao  walijipanga  kujitosa katika ulingo  wamedai  wamevunjika moyo na maandalizi ya zoezi hilo na hivyo kuamua  kuahirisha  kujitosa .

Kwani  walisema kwa miaka mingine zoezi hilo  huwa linafanyika katika hali ya uwazi mkubwa na maandalizi yake  huwa yanaanza mapema ila kwa mwaka huu hakuna kinachoendelea huku  siku  zikizidi  kuyoyoma.

Alisema mrembo Amina kuwa kuna uwezekano mkubwa wa shindano hilo kwa mwaka  huu  likakosa mvuto na hata mrembo atakayepatikana  kutouzika katika mashindano ya kanda  kutokana na maandalizi ya kiubabaishaji ambayo yanaendelea  kimya kimya.

" Tunashangaa  sana miaka mingine hadi sasa fomu kwa  washiriki  zinakuwa  zimetolewa na  kambi  limeanza  ila mwaka huu japo kusikia kuwa kambi lingeanza toka May 22 ila hadi  leo ni may 26  ila hakuna  kinachoendelea.....sasa  kuna maandalizi hapo ama  ubabaishaji"

Hata  hivyo  walimtaka muandaaji wa shindano hilo kwa mwaka huu  kuiga mfano wa muandaaji wa mashindano kama hayo mkoa wa Tanga  ambapo anatoa gari kwa mshiriki  wa shindano  hilo.

Jitihada za mtandao  huu kumtafuta mratibu wa shindano hilo  zinaendelea  ili kuweleza  sababu za kuchelewa kuanza maandalizi hayo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni