Wafanyakazi
wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania,tawi la jijini Arusha
wakiwa katika picha ya pamoja mara bada ya uzinduzi wa duka la huduma
kwa wateja leo.
......................................................................................................
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma za kibunifu nchini leo imezundua duka lake lakisasa lililopo jijini Arusha
Ufunguzi wa duka hilo ulizindulia na Mkuu wa wilaya ya Arumeru ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.
Akiongea
wakati wa uzinduzi Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja bi
Adriana Lyamba alisema” Leo tunazindua duka la pili la kisasa baada ya
kuzindua duka letu la Xpress lililopo Mlimani City mwishoni mwezi
ulipita. Hii ni kwasababu tunaamini katika kutoa na kuwapatia wateja
wetu huduma bora na za kifunibu na uzinduzi wa leo ni mwendelezo wadhamira yetu ya kuleta huduma za kisasa zinazowahakikishia wateja wetu usalama na huduma bora wakati wote”.
Tunawahakikishia
wateja wetu huduma bora kote nchini na kwa wakazi wa Arusha sasa
wataweza kufurahia huduma zetu katika mazingira bora na yaliyoboreshwa
zaidi.Duka hili limetengenezwa kwa kisasa likiwa na uwezo wa kuwawezesha
wateja kupata huduma kwa urahisi bila usumbufu huku wafanyakazi wetu wakipata mazingira bora ya kufanyia kazi na kuleta ufanisi mkubwa.”
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bwana Nyirembe Munasa alisema”
Nawashukuru sana Airtel kwa kuongeza wigo kupitiia huduma kwa wateja na
kuleta mabadiliko ya kibunifu. Tunaamini ubunifu huu utaleta hari kwa
wafanyakazi na pia na kuongeza nafasi za ajira lakini sambamba na hayo
pia utawawezesha wakazi wa Arusha kupata huduma bora wakati wote na kwa
hilo Tunawashukuru sana Airtel”
Natoa
wito kwa wakazi wa Arusha na wateja wa Airtel kutembelea duka hili la
Airtel Xpress na kufurahia huduma na bidhaa za kisasa ikiwemo huduma ya
Airtel Money inayotoa suluhisho kwa mahitaji yao ya huduma za kifedha
ikiwemo kufanya malipo na kutuma pesa kirahisi zaidi aliongeza Munasa
Airtel itaendelea kuzindua maduka yake nchi nzima ili kufanya sehemu za kutoa huduma zao kuweza kufikiwa kirahisi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni