HOPE SERVICE STATION

nsekwa

ALTEZA

Jumatatu, 26 Mei 2014

CECAFA NILE BASIN CUP: AL-MERREIKH WAZOMEWA KWA KUTOKA SULUHU, POLISI `ZENJI MDOBWEDO`, MBEYA CITY `LAIVU` NA AFC LEOPARD USIKU WA LEO


44593hp2Al-Merreikh walizomewa baada ya suluhu
Na Baraka Mpenja wa fullshangwe, Dar es salaam
WENYEJI wa michuano ya CECAFA Nile Basin Cup, Al-Merreikh ya Sudan jana wamelazimisha suluhu pacha ya bila kufungana katika mechi ya kundi A dhidi ya Victoria University kutoka Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa ya Afisa habari wa CECAFA, Rodgers Mulindwa, mashabiki wa Al-Merreikh waliwazomea wachezaji wao baada ya kipyenga cha mwisho kupigwa kuonesha kuwa hawajaridhishwa na suluhu hiyo.

Kocha wa klabu Al-Merreikh, Mjerumani, Martin Otto Pfister alikiri kubanwa zaidi na wapinzani wao na kusema kuwa kwa muda wote wapinzani wao waliharibu mipango yao.

“Kiufundi wako vizuri sana (Victoria University). Walicheza kwa jitihada kutunyima nafasi za kushinda. Waliharibu mipango yetu na kutupa nafasi kidogo ya kucheza mpira”. Alisema kocha huyo Mjerumani aliyefanya kazi Afrika tangu miaka ya 90.

Suluhu ya jana imeifanya Victoria University kuwa mshindani wa kombe kwasababu timu zote zimefuzu hatua ya mtoano,  huku zote zikiwa na mechi moja mkononi.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni