Chama Cha Walemavu mkoani Iringa CHAWATA kimeonekana kupiga hatua baada ya kujenga
daraja la kuelekea katika ofisi zao.
Akizungumza
na mtandao huu wa www.matukiodaima.com
ofisini kwake Katibu wa Chama Cha Walemavu Mkoani Iringa Bwana Haruna Mbata
alisema kuwa toka wameingia madarakani mwezi wa kwanza mwaka huu walikuwa na
mipango mingi sana mmoja wapo ni huo wa kujenga daraja la kuingilia ofisini
kwao ambapo wameweza kulitimiza lengo hilo.
“tulikuwa
na mikakati mingi mmoja wapo ulikuwa ni huu wa kutengeneza hilo daraja hapo nje
maana watu wanashindwa kupita hapo hasa watu wenye ulemavu wanapokuja kujadili
mambo ya vikoba vyao na ndipo tukaamua tulijenge haraka hili daraja hivyo
tukafanya harambee ambapo mgeni rasmi alikuwa Meya wa Manispaa ya Iringa Amani
Mwamwindi ambapo tulichangisha michango na tukapata ela ya kujengea hili
daraja.” Alisema Mbata.
Hata
hivyo alisema baada ya kukamilisha daraja kwa sasa wana mpango wa kutengeza
choo kwa ajili ya matumizi ya watu walio na ulemavu ambapo wakimaliza choo
watajenga ofisi ambayo itakuwa ikitumika na wao wenyewe na kusema wanataka
wabadilishe mazingira ya ofisi yao yaweze kutumika na kila mtu hususani kwa
watu walemavu.
“kuna
ofisi nyingine unakuta mtu mlemavu hawezi kuingia ndani anaishia nje tu ofisi
inakuwa ina ngazi nyingi kitu ambacho kinampelekea kushindwa kufanikisha
kilichompeleka sasa hapa tunataka tuweke mazingira ambayo yatamfanya mtu wa
aina yeyote ile aweze kuingia na kufanikisha kile kilichomleta.” Alisema
Pia
amewashukuru wananchi kwa kushirikiana nao mpaka wamefanikisha kujenga daraja
hata hivyo alitoa wito kwa serikali na wananchi kwa ujumla kuona kuwa kuna
mahitaji muhimu kwa walemavu na kushirikiana nao ili kuweza kujenga Taifa la
kesho.
NA
DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni