Na Wiliam Bundala mwandishiwetublog kanda ya ziwa.
Watu saba kati ya 100 Kijiji cha Kenyamanyori, Kata ya Turwa,
Wilaya ya Tarime walioshiriki kunywa dawa ya mganga wa kienyeji
aliyeletwa kutoka Busia nchini Kenya wameingia kwenye wakati mgumu baada
ya kushindwa kutimiza masharti ya kulipa Sh3 milioni kila mmoja.
Wanakijiji
hao walikusanyika juzi asubuhi baada ya kengele ya kijiji kugongwa na
uongozi, huku wakieleza kwamba ilikuwa siku ya nne kwa kengele hiyo
kugongwa lengo likiwa ni kuzungumzia wizi unaoendeshwa na watu
wasiojulikana.
Inadaiwa
wizi wa kuvunja maduka umekithiri kijijini hapo, baada ya wanakijiji
hao kuwasili eneo la mikutano, walielezwa kusudio la kengele kuwa
ilikuwa ni kutokana na kukithiri kwa matukio ya uhalifu.
Miongoni
mwa waliovunjiwa duka ni Ayubu Wambura, anayedaiwa kuleta mganga kutoka
Busia nchini Kenya kuwabaini wahusika, hivyo kila mmoja aliombwa kunywa
dawa ya mganga huyo au kuacha maana ni hiyari.
Hata hivyo, walitahadharishwa kwamba kama aliyeshiriki hatakunywa dawa hiyo, itamuumbua maana aliyeibiwa atakuwa amekunywa.
Kabla
ya kuanza kunyweshwa, mganga huyo aliomba wanakijiji iwapo kuna
mhusika, ni vyema ajitokeze kabla ya kuingia gharama za kuwarejesha hali
yao ya kawaida hazijaongezeka watakaponaswa.
Hata hivyo, wanakijiji walidharau wakidai ni mbabaishaji huyu hawezi lolote kwani hivyo ni vitisho.
Ilipotimu
saa 5:00 asubuhi, mganga aliwaeleza ndani ya saa mbili tangu mtu anywe
dawa yake atakuwa ameanza kuonyesha vitendo alivyokuwa akifanya wakati
anaiba dukani.
Saa
6:00 mchana tayari dalili zilikuwa zimenza kuonekana kwa watu saba
wakiwamo wafanyabiashara wenzake, pia yumo mwanamke wakiwa wamelewa
wanafanya vioja, huku wengine wakila nyasi na kutafuna midomo.
Wambura
alisema anachotaka ni kurejeshewa Sh12 milioni, zikiwamo gharama za
mganga huyo, huku walionaswa na dawa hiyo wakitakiwa kulipa Sh3 milioni
na kupewa siku tatu vinginevyo watageuzwa vichaa.
“Nimeibiwa
sana ila ninavumilia, hii ni mara ya tano sasa, nimechoka na
ninachotaka wanirudishie Sh12.5 milioni gharama niliyotumia ikiwamo mali
zangu walizochukua, waliwahi kunivamia na mke wangu tunatoka dukani
wakatukata mapanga hadi mke wangu akafa,” alisema Wambura.
Pia, tukio hilo lilishuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Vanance Mwamengo, madaktari wa Hospitali ya Mji wa Tarime, madiwani na polisi na kwamba kutokana na wananchi kutokuchukua sheria mkononi, masuala
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni