Habari zilizoufikia mtandao huu zinasema kuwa serikali ya mkoa wa Shinyanga imesitisha huduma ya fast Track katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambako hivi karibuni huduma za matibabu katika hospitali hiyo zimepanda mfano katika kupanda huko kwa huduma za matibabu akina mama walikuwa wanalazimika kujifungua kwa gharama ya shilingi elfu 70,na kama ni ulikuwa unahitaji kupasua jipu basi ingekulazimu kulipia hudum hiyo shilingi elfu 40.
Akitoa ufafanuzi kutoka kwa mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal aliyetaka kujua imekuwaje gharama za matibabu zikapanda katika hospitali ya mkoa bila kufuata utaratibu unaotakiwa,mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga amesema serikali kuanzia sasa imesitisha huduma hiyo kwa ajili ya maslahi ya wananchi na chama tawala kwani kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu kupanda kwa gharama za matibabu kupanda katika hospitali hiyo wakati wananchi wengi ni maskini.
Haya yamejiri wakati huu katika mkutano wa wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga unaoendelea
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni