HOPE SERVICE STATION

nsekwa

ALTEZA

Jumapili, 18 Mei 2014

DIAMOND ATAMBA KUTWAA TUZO MTV

………………………………………………………………….

MSANII nyota wa muziki wa kizai kipya nchini Naseeb Abdul ‘Diamond’ ametamba kufanya vizuri katika tuzo za MTV Africa ‘Mama’ zinazotarajiwa kufanyika Juni 7 mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Diamond ameingia katika tuzo hizo kwenye vipengele viwili ambavyo ni msanii bora wa Afrika pamoja na msanii mwenye nyimbo bora ya kushirikisha.

Wimbo ambao umembeba kwa kiasi kikubwa msanii huyo ni wa Number One aliomshirikisha Davido wa Nigeria ambapo amewaomba mashabiki wake kumpigia kura kwa wingi.



Akizungumza katika hafla ilioandaliwa na kituo cha runinga cha MTV Base kama sehemu ya kusherekea tuzo za MTV Africa mwaka huu iliyofanyika My 16,2014  kwenye Ukumbi wa Billcanas,jijini Dar es Salaam  Diamond alisema kuwa anafanya muziki wa Afrika na ndio maana amepata mafanikio makubwa. wasanii waliotumbuiza ni pamoja na Sauti Solo,Mi Casa Msic

Alisema kuwa wasanii wanatakiwa kujituma zaidi ili kuhakikisaha wanafikia malengo zaidi.
“Ninafanya muziki wenye ladha ya Afrika na hivyo ninatarajia kufanya vizuri zaidi katika tuzo za MTV nawaomba Watanzania wazidi kunipigia kura ili niweze kuibuka kinara, wasanii wanatakiwa kufanya juhudi za ziada kwa kutoa kazi nzuri ili kuhakikisha wanafikia malengo,” alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni