Mtu
mmoja afariki dunia na mwingine kushikiliwa na jeshi la polisi mkoani Iringa
katika matukio tofauti likiwemo la mtu asiyefahamika kwa jina kukutwa amefariki
dunia mara baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya miti iliyopo kwenye
korongo.
Akizungumza
na mtandao huu wa www.mwandishiwetublog.com ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoani hapa Ramadhani Mungi alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 21 mei majira ya saa 6 Mchana
huko maeneo ya kijiji cha Kitelewasi kilichopo kata ya Mbalamaziwa wilaya ya
Mufindi.
Kamanda
alisema marehemu ambaye jina lake halikuweza kufahamika ila ni jinsia ya kiume
aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 17-21 alikuwa amejinyonga kwenye korongo la
Ndengemakwaya na kusema chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa.
Wakati
huohuo, askari wakiwa doria walimkamata mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina
la Happines Charles (25) mkazi wa Mawelewele akiwa na dawa za kulevya aina ya
bhangi kete 97 zikiwa kwenye mfuko mweusi.
Tukio
hilo lilitokea mnamo tarehe 21 mei huko maeneo ya Makorongoni na kusema
mtuhumiwa huyo alikutwa na dawa hizo baada ya kufanyiwa upekuzi kwenye duka
lake huku chanzo kikiwa ni kipato kidogo.
NA
DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni