Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akiwahutubia wananchi katika moja kati ya mikutano yake
......................................................
Wito umetolewa kwa wazazi kupenda kuhudhulia vikao vinavyofanyika mashuleni pindi wanapopata taarifa za kuwataka wafike mahali hapo.
......................................................
Wito umetolewa kwa wazazi kupenda kuhudhulia vikao vinavyofanyika mashuleni pindi wanapopata taarifa za kuwataka wafike mahali hapo.
Akizungumza
na mtandao huu wa www.matukiodaima.com
ofisini kwake Afisa Elimu wa Shule za Msingi Manispaa ya Iringa Halfani
Masukira alisema kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa hawahudhulii vikao vya shuleni
mwa watoto wao na mwisho wa siku wanakuja kulaumu kuwa shule ina michango
mingi.
“baadhi
ya wazazi hawapendi kwenda kusikiliza walichoitiwa mashuleni na mwisho unakuta
wanalalamika kuwa michango mingi inatoka wapi, bila kujua kama angeenda
kusikiliza alichoitiwa angejua ni kwanini wanatakiwa kuchangisha hiyo michango
hivyo ili kumaliza haya maswali nawashauri wazazi wote wanapoitwa mashuleni
basi wafike bila kukosa ili kujua maendeleo ya watoto wao na pia kujua kamati
ya shule inasemaje na pia kutoa maoni yao kama wanaona mchango huu haufai au
vipi” alisema bwana Masukira.
Pia
aliwataka walimu kutojiamulia kitu bali wawasubiri wazazi wote wafike na
wajadiliane kwa pamoja kuhusu michango na wakubaliane kwa pamoja na sio wapange
wenyewe michango halafu waje wawape wazazi barua tu bila kuwashirikisha katika
vikao vyao.
Na
kwa upande wake Afisa Taaluma wa Shule za Msingi Manispaa ya Iringa bwana Salmin Mndeme alisema kuwa sio shule
zote zinawataka wazazi watoe michango mingi bali inatokana na shule yenyewe kama
ina vitu vitakavyopelekea kutakiwa
kulipia basi lazima kutakuwa na michango mingi.
“michango
mingine inategemeana na mahitaji ya shuleni hapo, unakuta shule ina maji,
mlinzi na vitu vingine hivyo inawafanya walimu wachangiane na wazazi katika
kulipia hivyo vitu na ndo maana unakuta michango inakuwa mingi.
Lakini sisi kama manispaa mfano walimu wakikaa vikao vyao huko mashuleni na wakafanya bajeti yao ya mwaka kama kamati ya shule wakituletea sisi hapa tuangalie bajeti yao kama tukiona wamezidisha michango basi sisi tunawaambia wapunguze baadhi ya vitu ili bajeti ipungue ili wazazi waweze kuchangia michango hiyo kwani kuna wazazi wengine hawana uwezo wa kuchangia michango mingi na ndio maana tunawaambia walimu wapunguze hiyo michango walioiweka katika bajeti zao za mwaka.” Alisema bwana Mndeme.

Manispaa
ya Iringa imejitahidi kwa mwaka huu imeweza kushika nafasi ya tano Kitaifa kwa
kufaulisha vizuri wanafunzi waliomaliza Elimu ya Msingi Tanzania nzima.
NA
DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni