Shirika rasmi la habari nchini Uchina Xhinua limesema kuwa serikali imewaondoa zaidi ya raia wake 3000 kutoka nchini Vietnam kufuatia ghasia dhidi raia wa Uchina nchini humo.
Serikali mjini Beijing inaandaa safari nyingine za ndege huku naibu waziri wa maswala ya kigeni Liu Jianchao akizuru Vietnam kwa mazungunmzo na mamlaka.
Aidha waziri huyo amewatembelea baadhi ya raia wa Uchina waliojeruhiwa hospitalini.
Wanaharakati nchini Vietnam wameitisha maandamano zaidi dhidi ya raia wa Uchina hii leo licha ya mwito wa serikali wa kutaka kusitishwa kwa maandamano hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni