
Nyota wa mchezo: Sir Alex Ferguson akimpatia zawadi Angel Di Maria kama mchezaji bora wa mechi.
Imechapishwa Mei 25, 2014, saa 8:51 mchana
KIBABU Sir
Alex Ferguson alishindwa kuvumulia katika mchezo wa jana baada ya winga
wa Real Madrid, Angel di Maria kuonesha kiwango cha juu na kuamua
kumpa zawadi ya mchezaji bora wa mechi ya fainali ya UEFA mwaka huu.
Gwiji
huyo wa Manchester United alivutiwa sana na kiwango cha Di Maria
katika mchezo wa jana na kuisaidia Real Madrid kushinda mabao 4-1 dhidi
ya majirani zao, Atletico Madrid, mjini Lisbon.


Akikimbiza: Di Maria alikuwa nguzo ya Real Madrid usiku wa jana mjini Lisbon

Muda wa sherehe: Muargentina huyo alifanya kazi kubwa kuwasaidia Real Madrid kutwaa ndoo yao ya 10 ya Ulaya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni