Baadhi
ya wanachama wa Chama Cha mapinduzi (CCM) tawi la chuo cha kimataifa
cha Diplomasia wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa
uchaguzi wa tawi hilo jana jumamosi 24/5/2014.Kutoka kushoto ni Mohamed
Mkumbwa,George Fautine,Dk.Telesphory Kyaruzi,Faiza Salim,Kanali
Rankho,Mtela Mwampamba,Ali Makwiro na Kennedy Ndosi.Uchaguzi huo
ulisimamiwa na Mtela Mwampamba,Kanali Rankho,Dotto Nyirenda,katibu wa
CCM mkoa wa vyuo vikuu Bw.Zenda Daniel na katibu wa CCM itikadi na
uenezi wa mkoa wa vyuo vikuu Bw. Madebe,pia uliongozwa kwa kanuni zote
za chama hicho hadi mwisho ambapo ulimalizika saa tatu na nusu usiku.
Baadhi
ya vingozi wa tawi jipya la Chama Cha mapinduzi (CCM) la chuo cha
kimataifa cha Diplomasia wakiwa katika picha ya pamoja baada
ya kumalizika kwa uchaguzi wa tawi hilo jana jumamosi 24/5/2014 ambao
ulikuwa na ushindani mkubwa wa kisiasa hasa kutokana na chuo hicho kuwa
chimbuko la wanadiplomasia wanaoheshimika duniani pamoja na wanasiasa
machachari hapa nchini na Duniani kwa ujumla.Katika uchaguzi huo
Dk.Teresphory Kyaruzi alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa tawi hilo jipya
bila kupingwa,huku Bw.Kennedy Ndosi akichaguliwa kuwa katibu mpya wa
tawi baada ya ushindi wa kishindo dhidi ya mpinzani wake Severine
Kapinga aliyepata kura 3 dhidi ya 8 za wajumbe wote wa kamati kuu ya
tawi.
Kutoka
kushoto ni Ali Makwiro, Mtela Mwampamba, Dk.Telesphory Kyaruzi, Faiza
Salim, Mohamed Mkumbwa,Sixtus Muhaji,Kennedy Ndosi,George Fautine,Bonnah
Kalua,Kanali Rankho,George Lupenza na Dotto Nyirenda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni