Usajili
wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2014/2015) unaanza Juni 15 hadi
Agosti 3 mwaka huu wakati kipindi cha kutangaza wachezaji walioachwa au kusitishiwa
mikataba ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu.
Kipindi
cha kwanza cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi Julai 30
mwaka huu. Kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati ya Agosti 4 na 11
mwaka huu. Kuthibitisha usajili hatua ya awali ni Agosti 12 hadi 14 mwaka huu.
Usajili
hatua ya pili utakuwa kati ya Agosti 14 na 29 mwaka huu. Kupitia na kutangaza
majina ya pingamizi hatua ya pili ya usajili ni kuanzia Agosti 30 hadi Septemba
4 mwaka huu. Uthibitisho wa usajili hatua ya pili ni Septemba 5 na 6 mwaka huu.
Kwa
upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza Agosti 24 mwaka huu, na
ratiba inatarajiwa kutoka mwezi mmoja kabla (Julai 24 mwaka huu).
MECHI YA TAIFA
STARS YAINGIZA MIL 63/-
Mechi
ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Morocco
kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe iliyochezwa Jumapili katika Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 63,345,000.
Mapato
hayo katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Taifa Stars kuibuka na ushindi wa bao
1-0 yametokana na washabiki 11,079 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa
viingilio vya sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000.
Mgawo
wa mapato hayo ni asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni
sh. 9,662,796.61, gharama za kuchapa tiketi sh. 6,000,000, asilimia 15 ya
uwanja ni sh. 7,152,330.51, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 9,536,440.68
na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) kwa pamoja wamepata sh. 30,993,432.20.
WASHABIKI
KWENDA HARARE KUSHANGILIA STARS
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaandaa utaratibu utakaowawezesha washabiki
kwenda jijini Harare, Zimbabwe kushuhudia mechi ya Taifa Stars.
Mechi
hiyo ya marudiano ya Kombe la Afrika kwa ajili ya fainali zitakazochezwa
Morocco mwakani itafanyika Jumapili (Juni 1 mwaka huu) jijini Harare.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilishinda mechi ya kwanza
iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0.
Usafiri
huo utakuwa wa basi ambapo washabiki wanatarajiwa kuondoka siku ya Ijumaa na
kuwasili Jumapili mchana jijini Harare ambapo watashuhudia mechi na kuanza
safari ya kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo.
Washabiki
wanatakiwa kuwa na hati za kusafiria (pasipoti), nauli ya kwenda na kurudi
itakuwa sh. 300,000.
TIMU YA U15
YAWASILI GABORONE
Timu
ya Tanzania ya umri chini ya miaka 15 imewasili salama jijini Gaborone,
Botswana kwa ajili ya michezo ya Afrika ambapo itacheza mechi yake ya kwanza
Mei 22 mwaka huu dhidi ya Mali.
Kikosi
hicho cha wachezaji 16 chini ya Kocha Abel Mtweve kimetua jijini Gaborone jana
(Mei 19 mwaka huu) jioni kwa ndege ya South African Airways. Michezo hiyo itamalizika
Mei 30 mwaka huu.
Wachezaji
waliopo kwenye kikosi cha Tanzania ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli,
Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance
Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro
Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.
Nchi
nyingine zinazoshiriki michezo hiyo kwa upande wa mpira wa miguu ni Afrika
Kusini, Botswana, Nigeria, Mali na Swaziland.
Gabon
na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ambazo nazo zilikuwa zishiriki kwenye
michezo hiyo katika dakika za mwisho.
NGORONGORO HEROES YAENDA NIGERIA
Kikosi cha timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) chenye watu
25 kinaondoka kesho alfajiri kwenda Nigeria kwa ajili ya mechi ya marudiano
dhidi ya Nigeria (Flying Eagles).
Mechi hiyo
itachezwa Jumamosi (Mei 24 mwaka huu) katika Jiji la Kaduna kwenye Jimbo la
Kaduna ambalo lipo katikati ya Nigeria. Msafara wa timu hiyo unaoongozwa na
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Ayoub Nyenzi unaondoka kwa ndege ya Ethiopian Airlines.
Ngorongoro
Heroes inayonolewa na Kocha John Simkoko ilipoteza mechi ya kwanza iliyofanyika
nyumbani jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-0.
Mwamuzi
Alhadi Allaou Mahamat wa Tchad ndiye atakayechezesha mechi hiyo. Atasaidiwa na
Issa Yaya, Alfred Madjihoudel na Idriss Biani wote kutoka Tchad. Kamishna ni
Aboubakar Alim Konate wa Cameroon.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni