Mgeni rasimi katika uzinduzi wa tawi la
wanafunzi vyuo vikuu wanachama wa chama cha Kiswahili
Afrika Mashariki (CHAWAKAMA)afisa utamaduni mkoa wa Iringa Kenneth
Komba wa tano waliosimama kutoka kushoto akiwa na wanachama wa chama
hicho tawi la chuo kikuu cha Iringa mara baada ya kuzindua tawi hilo
...................................................................................
WANAFUNZI wa chuo kikuu cha Iringa zamani Tumaini wamewataka
wajumbe wa bunge la katiba kuhakikisha wanapigania lugha ya
Kiswahili ili iweze kupewa nafasi kubwa katika katiba mpya.
Rai
hiyo imetolewa na mlezi wa wanafunzi wa chama cha Kiswahili
Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Tullah Tweve wakati wa uzinduzi wa tawi
hilo chuoni hapo jana
Tweve
alisema kuwa hakuna faida kubwa kwa taifa kama kutumia lugha ya
Kiswahili kama lugha kuu katika taifa na hata kuitumia katika
kufundishia mashuleni na vyuo.
Alisema
wakati huu ni wakati mzuri wa Taifa kuweza kurekebisha makosa
yaliyokuwepo katika kuchanganya lugha na kukumbatia lugha za mataifa
mengine na kuacha lugha yetu .
Hata
hivyo alisema kuwa yeye kama mwalimu wa Kiswahili katika chuo
hicho moja kati ya mambo ambayo anayapa kipaumbele ni pamoja na
kiswahili kupewa kipaumbele.
Kwa
upande wao wanafunzi wanachama wa Chawakama walisema kuwa
walengwa wakuu wa chama hicho ni wanafunzi wa vyuo vikuu
wanaosoma Kiswahili na kuwa wanachama ni nchi tano barani Afrika kama
Tanzania ,Uganda , Kenya
,Rwanda na Burundi lea kusihiriki makondamano mbali mbali barani
Afrika .
Pia
walisema kuwa msukumo wa kuanzisha Tawi hilo ulitokana na jitihada za
mwalimu Tulla Tweve na Albart Chalamila na kuwa tawi kwa sasa
linawachama zaidi ya 60.
Walisema
kuwa chama hicho kimeanzishwa mwaka 2002 na kuwa katika chuo cha
Iringa tawi hilo lilianzishwa mwaka 2010 na kuwa mbali ya kutokuwepo
kwa tawi ila bado wanafunzi wa somo la kiswahili waliende
Aidha
walisema changamoto kubwa ni kukosekana kwa fedha za kuendeshea
chama pamoja na chama hicho kutotambulika kwa kuwa na uongozi wa
unaojulikana na chuo hicho.
Afisa
utamaduni mkoa wa Iringa Keneth Komba mbali ya kuwashukuru wanachama
wa chama hicho cha Chawakama kwa kuenzi kiswahili bado alisema
kuwa jitihada hizo kubwa zilizoanzishwa na chuo hicho.
Hata
hivyo alisema kuwa wenye uwezo wa kukuza kiswahili ama kubomoa
lugha ya kiswahili ni wasomi wenyewe ambao wamepelekea kuyumbisha
lugha .
Komba alisema kuwa mikataba mibovu ya kifisadi katika Taifa inasababishwa na lugha ya kiingereza ambayo wengi wa
"Tunatambua
kuwa duniani kuna lugha zaidi ya 16 ikiwemo lugha ya kiingereza
,kifaransa kirusi na kiarabu na lugha mbali mbali huku
katika afrika lugha kuu ni kiswahili ambao lugha hiyo imekuwa
ikiendelea kukua zaidi barani afrika "
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni