Baadhi ya mabango yanayopinga harakati za Ukawa yakioneshwa katika mkutano huo |
Wakiwa na mabango yao mbele ya askari wa FFU |
Profesa Lipumba akisisitiza jambo katika mkutano wake huo |
Winfreda Ngoti akiuliza swali katika mkutano huo |
UMOJA
wa katiba ya Wananchi (Ukawa) umepokewa kwa mabongo yanayosisitiza umuhimu wa
serikali mbili katika mkutano wao uliofanyika jana, mjini Mafinga.
Ukiwa
na wazee na wanawake wachache, mkutano huo uliohudhuriwa na vijana wa kiume zaidi
ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni Mwenyekiti
mwenza wa Ukawa.
Wengine
waliohutubia ni pamoja na mwakilishi wa chama cha NCCR-Magezuzi, Danda Juju na
kiongozi wa taasisi ya kiislamu ya Shura ya Imamu, Rajabu Katimba.
Baadhi
ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na vijana hao yalikuwa na ujumbe uliosomeka “vijana
Mafinga tuna mashaka na ndoa ya Ukawa, watauza nchi” na bango la waendesha
bodaboda lilisomeka “ Rudisheni posho kwanza mjengoni dodoma.”
Mengine
na ujumbe wake kwenye mabano ni lililowatambulisha wafanabiashara wa sokoni
lililosomeka “Mafinga Sokoni, serikali tatu sio suluhisho la matatizo ya
wananchi”, na la wapiga debe Mafinga stendi lilisomeka “Karume Oyee, Nyerere
Oyee, Muungano Saafi.”
Bango
la waliojitambulisha kuwa ni machinga lilisomeka “tunataka serikali inayojali
wajasiliamali, sio kujali matumbo yao”, na lile la wakulima lilisomeka “kilimo
kwanza, utaifa kwanza.”
Wakati
mabango hayo yakizungushwa katika mkutano huo muda ambao Profesa Lipumba
alikuwa akihutubia, usikivu ulipotea kwa dakika takribani 15 hadi 20 baada ya
sehemu ya kundi la vijana lililokuwa likimsikiliza kuelekea upande waliokuwa vijana
wenye mabango hayo.
Polisi
waliokuwepo walilazimika kuingilia kati kadhia hiyo na mzozo baina yao na
vijana waliokuwa na mabango hayo ulisikika.
Mmoja
wa Polisi aliyekuwa akiwatuliza vijana hao alisema “Jamani huu ni mkutano
halali wa kisiasa, achene wenzenu wafanye mkutano wao; yatoeni mabango yenu.”
Mmoja
wa vijana aliyekuwa amebeba bango mojawapo jina halikupatikana mara moja
alisikika akisema “Ukawa sio chama cha siasa, wao wana mtazamo wao na sisi tuna
mtazamo wetu, kwahiyo sio jambo la ajabu wakajua kwamba Mafinga wengi hatuwaungi
mkono na sio dhambi kuonesha hisia zetu katika mkutano wao.”
Akielezea
vurugu hizo, Profesa Lipumba alisema zinafanywa na vijana waliotumwa na Chama
cha Mapinduzi (CCM) kwasababu ya msimamo wao wa kutaka serikali mbili, tuhuma
zilizokanushwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu aliyehojiwa
baaada ya mkutano huo.
“Siamini
kama mkutano huu ungekuwa unahutubiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Taifa Jakaya
Kikwete wangekuja na mabango hayo na kufanya vurugu hizi?” alisema na sauti
kutoka kwa baadhi ya vijana hao zikasikika zikisema.
“Kama
angekuja na msimamo wa serikali tatu ni lazima angekutana na mabango haya; sisi
tunataka serikali mbiliii.”
Hata
baada ya vurugu hizo kupoa na Profesa Lipumba kuruhusu maswali baada ya
kufafanua sababu mbalimbali zilizosababisha wasusie bunge la Katiba na
kuanzisha Ukawa, mkutano huo ulitaka kuvurugika tena.
Swali
lililotaka kuuvuruga mkutano huo lilitoka kwa kijana aliyejitambulisha kwa jina
la Rashid; Rashid alitaka kujua kwanini CCM hawapo katika umoja huo.
Pamoja
na vijana wengine kupiga kelele wakiashiria kwamba hilo sio swali, Profesa
Lipumba alijibu akisema ni swali zuri.
Alisema
milango ya Ukawa ipo wazi kwa mtu yoyote ndani nan je ya bunge la Katiba
wakiwemo wabunge na viongozi wa CCM.
“Tutafurahi
kuwapata wana CCM, tunawakaribisha Ukawa ili kwa pamoja tushirikiane kupata
Katiba inayotokana na wananchi,” alisema.
Mwingine
aliyeuliza swali alikuwa Winfreda Ngoti aliyesema harakati za kudai serikali
tatu hazitakuwa na maana yoyote kama matatizo ya wananchi hayatashughulikiwa.
“Watanzania
wana matatizo lukuki, vituo vya huduma za afya havina wataalamu, dawa, wakulima
hawapati pembejeo kwa wakati na bei zake ni kubwa, wafanyabishara wadogo
wanabanwa na kukamuliwa kodi, walimu hawapati mishahara kwa wakati, askari wana
mishahara midogo na wanakula rushwa,” alifafanua.
Katika
majibu yake, Profesa Lipumba alisema hayo yote yatafanyiwa kazi kukiwa na
Katiba bora itakayosisitiza uwajibikaji na uadilifu.
Alisema
rushwa na ufisadi vimekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya taifa hili katika
sekta zote zikiwemo elimu, afya, kilimo, biashara, miundombinu na zinginezo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni