Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Magubike Bi Lenatha Mbilinyi kushoto akipokea msaada wa saruji mifuko 100 kutoka kwa mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa leo ,wanaoshuhudia kulia ni katibu menezi wa CCM wilaya Denis Lupala na diwani wa kata ya Nzihi katikati Bw Stivin Mhapa
........................................................................................
MBUNGE wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa ameanza kutimiza ahadi zake kwa wananchi wa jimbo la kalenga kwa kukabidhi mifuko zaidi ya 150 ya saruji katika kijiji cha Magubike na kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2.5
Saruji hiyo mifuko 100 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa jengo la utawala shule ya sekondari Dimitrios katika kijiji cha Magubike na mifuko 50 kwa ajili ya shule ya sekondari Kidamali.
Mgimwa alisema kuwa lengo la kutimiza ahadi yake hiyo ni kama njia ya kuwashukuru wana Kalenga kwa kumchagua katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni pia kutimiza ahadi mbali mbali binafsi ambazo alizitoa mbunge aliyefariki marehemu Dr Wiliam Mgimwa.
Alisema ataendelea kutimiza ahadi binafsi zilizotolewa na marehemu Dr Mgimwa kulingana na uwezo wake na zile za kitaifa ambazo zipo katika Ilani ya CCM atahakikisha anaikumbusha serikali ya CCM ili kutimiza ahadi hizo kwa wakati.
“Ndugu zangu wananchi mbali ya kuwa ubunge wangu ni wa mwaka mmoja ila tayari mimeanza kutimiza ahadi bila ya kuchelewa na ninawahakikishieni sita waangusha nitaendelea kufanya hivyo zaidi mniombee uzima”
Alitaja maeneo ambayo tayari amekabidhi ahadi zilizotolewa na mbunge aliyefariki kuwa ni pamoja na Kiwere shule ya msingi mifuko 80 ya saruji,shule ya msingi wangama bati 100 na saruji mifuko 50,shule ya msingi Negabii bati 100 ,shule ya msingi Mibikimitali bati 50 ,Kijiji cha Isupilo bati 50 na saruji mifuko 50 na maeneo mingine mengi.
Pia amekabidhi kiasi cha Tsh 500,000 kwa ajili ya kuchangia kuwezesha kusajili timu ya kata ya Nzihi na nyingine kwa ajili ya ukarabati wa soko
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni