HOPE SERVICE STATION

nsekwa

ALTEZA

Ijumaa, 6 Juni 2014

WANANCHI KATA YA NZIHI JIMBO LA KALENGA WAMPONGEZA MBUNGE MGIMWA WASEMA NI MBUNGE HAWATAKI MWINGINE, MWENYEWE AWATAKA KUTOA USHIRIKIANO ZAIDI

Wazee kijiji cha Nyamihuu wakimpa baraka na kumpongeza mbunge  Mgimwa  kwa uchapa kazi wake 
MBUNGE  wa jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa amesema atahakikisha anafanya kazi na  vyama  vyote vya  siasa na  kuwa kuwataka  wananchi wa  jimbo la Kalenga kuachana na makundi  ya vyama vya siasa na kuunagana  pamoja  ili  kufanikisha  jimbo hilo kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo.

Mbali ya  kuwataka kuachana na makundi  ya kisiasa  pia amewataka  waliokuwa  wagombea  wa nafasi za ubunge katika uchaguzi mdogo  kupitia  CCM kuacha  kujipitisha  kwa  sasa kwa  wananchi na badala yake kusubiri uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Akizungumza kwa nyakati  tofauti katika  mikutano yake ya hadhara  kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa  kumchagua na leo katika kata ya Nzihi ,mbunge huyo  alisema kuwa amelazimika  kuomba ruhusa bungeni kwa  spika  ili kurudi  kuwashukuru  wananchi hao hasa  kutokana na upendo mkubwa ambao  wananchi wa jimbo hilo  walionyesha kwake.

"Ndugu  zangu nilianza  kuzunguka katika baadhi ya maeneo  na kutekeleza ahadi  mbali mbali hata kabla ya  kuapishwa  rasmi  bungeni ......na nitajitahidi kulingana na uwezo wangu  ili kuona natimiza wajibu  wangu kwenu na kamwe  sitawaangusha ndani ya bunge na nje ya  bunge"

Hivyo  aliwataka  wananchi  kwa umoja  wao kuendelea  kumuombea afya  njema  ili kufanikisha  kutimiza ndoto  yake ya  kufikisha maendeleo  katika  jimbo hilo ikiwa ni pamoja na kutimiza sehemu kubwa ya ahadi ambazo zilitolewa na marehemu Dr Wiliam Mgimwa aliyekuwa  mbunge  wa  jimbo  hilo.

Kuhusu  suala la kuyawezesha makundi mbali mbali Mbunge Mgimwa  aliwataka  wananchi  kujiunga na vikundi  vya VICOBA ili  kuviwezesha  vikundi  hivyo  kiuchumi zaidi badala ya  kuwa mtu mmoja mmoja na kuwataka  wazee  pia  kuanzisha umoja  wao na  kupeleka mahitaji yao katika  ofisi  yake.

"Kuna  vikundi  vya VICOBA ambavyo tayari  vimeanzishwa na   moja kati ya  vikundi  hivyo  tayari  nimechangia kiasi  cha Tsh 500,000 na nitaendelea  kuchangia na kuna eneo ambalo marehemu mbunge wetu aliyepita aliahidi kuchangia milioni 1 katika  kikundi cha VICOBA Magubike nasema  fedha  hizo  nitazitoa  mimi "

Alisema  kuwa tayari ameanza  kupigania  suala la umeme na maji katika  vijiji  vya jimbo la Kalenga  bungeni na kuwa  mawaziri wa  wizara  hizo  wameahidi  kulifanyia kazi na kuendelea kusaidia miradi hiyo mikubwa ambazo ndizo ahadi  kubwa  zaidi.

Awali  wananchi  wa kijiji cha Magubike  walimpongeza mbunge  huyo na  kuwa katika historia ya  jimbo la Kalenga  hawajapata kuwa na mbunge mkweli na mchakakazi kama  huyo na kurudi mapema zaidi kwa wananchi kuwashukuru na hivyo kumhakikishia  kuwa hawana mpango wa kumchagua mbunge mwingine mwaka 2015 na kukiomba chama cha mapinduzi kumbariki kuendelea  kuongoza jimbo hilo .

Kwa  upande  wake katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Iringa Denis Lupala alisema  kuwa utendaji kazi mzuri wa mbunge  huo ndio ambao unakishawishi  chama kuendelea  kumpa ushirikiano zaidi na kuwa wananchi hawana sababu ya kubabaishwa na wapinzani ambao  wameanza kujipitisha katika  jimbo hilo.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni