Baadhi ya washiriki wa shindano la Redds Miss Iringa 2014 ambao kesho watapanda ulingoni kuwania taji hilo |
mratibu wa Redds Miss Iringa 2014 Victor Chakudika akizungumza na mtandao huu wa matukiodaima ofisini kwake leo
.................................................................................................................................................
MKUU wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma kuungana na wakazi wa mkoa wa Iringa kumshuhudia mrembo atakayevishwa taji la Redds Miss Iringa 2014.
Katika kinyang'anyiro hicho kinacho kutanisha warembo 11 kutoka chuo kikuu cha Iringa ,Ruco na vyuo vingine vya mkoa wa Iringa na warembo wakali kutoka nje ya vyuo ,mkuu huyo wa mkoa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo itakayofanyika usiku wa kesho ijumaa katika ukumbi wa St Dominic .
Awali shindano hilo lilipangwa kufanyika Juni 6 mwaka huu lilikwama kufanyika baada ya mratibu wake aliyepewa kibali na kamati ya Redds Miss Tanzania kuingia mitini bila ya kufanyika kwa onyesho .
Kutokana na hali hiyo ili kunusuru mkoa wa Iringa kukosa mwakilishi katika shindano la Redds Miss Tanzania kamati ya Redds Miss Tanzania chini ya mratibu wake Hashim Lundenga walilazimika kumpa mratibu mpya kutoka kampuni ya Chakudika Intertainment chini ya mkurugenzi wake Victor Chakudika ambaye ni Meneja wa kituo cha radio ya Nuru Fm ya mkoani Iringa .
Hata hivyo kampuni hiyo imeweza kufanya kazi hiyo ya kuhakikisha inafanya maandalizi makubwa ya kusaka warembo na wadhamini ambao wangewezesha shindano hilo kufanyika .
Akizungumzia maandalizi ya shindano hilo mratibu wa kampuni hiyo Chakudika alisema maamuzi ya kuandaa shindano la Redds Miss Iringa kwa lengo a kutopoteza vipaji vya mabinti waliokuwa tayari kushiriki shindano hilo na kuondoa aibu ya mkoa wa Iringa kutopelekwa mwakilishi katika shindano la Redds Nyanda za Juu ambako wamekuwa wakishiriki kila mwaka.
Alisema kuwa shindano la Redds Miss Iringa limekuwa chachu ya ajira kwa mabinti wengi mkoani hapa kwa kuweza kutangaza vipaji vya washiriki wanaojitokeza kushiriki kila mwaka.
Chakudika alisema shindano hilo linatarajia kuwa la kisasa kutokana na maandalizi yake kuendelea vyema na kuwataka wadau wa tasnia ya urembo ujitokeza kwa wingi katika ukumbi wa St. Dominic likalofanyika shindano hilo.
Aliongeza kuwa hadi sasa warembo 11 wamejitokeza kushiriki shindano hilo na wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Hotel ya Gentle hill ya mjini hapa.
Aidha msanii Mo Music anayetamba na wimbo wake wa ‘Basi Nenda’ anatarajia kutoa burudani kali katika shindano hilo ,wasanii wengine chupukizi wa mjini Iringa, vikundi vya sanaa, Wakali wa Kudance wa mjini Iringa.
Aliwataja wadhamini wa shindano hilo licha ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds, wengine ni Nuru Fm, kampuni mpya ya mabasi ya Sutco High Class, Gentle Hills na kuwataka wadau zaidi kujitokeza kudhamini shindano hilo.
Chakudika alisema kuwa kiingilio ni kati ya Tsh 10000 na 20,000 kwa V.I.P na mshindi wa taji hilo ataondoka na fedha kiasi cha Tsh 500,000 ,mshindi wa pili atapewa Tsh 300,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa kiasi cha Tsh 200,000 wakati washiriki wengine wote watapata kifuta jasho cha Tsh 100,000 kila mmoja .
Usikose kushuhudia Redds Miss Iringa 2014 mtandao huu utarusha moja kwa moja hapa kesho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni