Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Baba watoto Center Bw.Mgunga Mwamnyenyelwa kilichopo mburahati kwa jongo wilaya ya kinondoni Dar es salaam, akizungumzia juu ya kituo hicho kinavyo fanya kazi na sababu za kuwakusanya watoto hao katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kuwajengea uelewa zaidi na kuwafundisha vitu mbalimbali kama Ngoma, Sarakasi, ushonaji ili baadae waweze kuja kujitegemea wenyewe.
Meneja mradi wa Fit For Life Habiba Issa akielezea kwa kina juu ya Mradi huo pamoja na malengo yake
Daniela Titze International Relation Fit For Life
Mani kutoka Ujerumani na ambaye pia ni Mwalimu wa Ngoma ya Brazil Samba Rege akielezea mafanikio na jinsi mafunzo yanavyo endelea.
Kikundi cha ngoma ndani ya kituo cha Baba watoto pamoja na wanafuzi waki achia burudani ya muziki aina ya Samba Rege
Mwalimu Daudi akiwa ana piga ngoma aina ya Samba Rege
Moja ya mambo yanayo fanywa katika kituo cha baba watoto utengenezaji wa maleba(costumes)
Vijana wakiwa katika mazoezi
Vijana wakifanya mafunzo ya serekasi katika kituo cha Baba watoto center
Kituo cha kusaidia watoto waishio katika mazingira magumu cha Baba watoto
center kupitia mradi wa FIT for –LIFE kinacho endesha mafunzo ya sanaa kwa
watoto walio kati ya umri wamiaka 10 hadi 15 mpaka 25 aina ya mafunzo yanayo
tolewa na pamoja na sarakasi ,muziki wa aina ya samba rage,kituo hicho
kilichopo wilayani kinondoni ambapo
mradi huo ni wamiaka mitatu kutoka mwaka
2013 hadi mwaka 2016
Akizungumza na waandishi wa habari katika warsha iliyo andaliwa kwaajiri
kuwafundisha vijana ambao nimaalumu kwaajili ya kuwa waalimu watakao weza
kuwafundisha wanafunzi katika kituo
hicho mkurugenzi mtendaji wa kituo Ndugu Mgunga Mwamnyenyelwa ameeleza jinsi
kituo hichokilivyo weza kuanzishwa katika maeneo ya mburahati na wakazi wa maeneo hayo kuweza kufaidika na
kituo hicho ,vilevile ameeleza changamoto wanazo kumbana nazo katika kituo
hicho,
Mradi huo wa FFL unao fadhiliwa na umoja wa ulaya (EU) ambao
unaendeshwa kwa hisani ya
Goethe-Institute kama msimamizi mkuu amapo meneja wa mradi Habiba Issa ameeleza
jinsi mradi huo unavyo endeshwa ikiwa lengo la mradi huu ni kuendeleza kukuza
kwa vipaji kwa vijana na kuweza kujipatia fura mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuwa mwalimu katika sehemu tofauttofauti za mradi huo
Aidha meneja huyo bi. Habiba Issa amesema kuwa wameamua kuanzisha mrahi huu
wa ili kuweza kuwasaidia vijana hususani walio maliza katika viwango mbalimbali
vya elimu kwani wameweza kuwaandalia mazingira mazuri ya kujifunza
uselemala,utengenezaji wa maleba
(costomes)kwaajili ya sanaa,uandaaji wa jukwaa(stage desgn) na matumizi ya
mfumo wa sauti na mwanga katika maonyesho ya sanaa.
Hata hivyo mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Baba watoto Bw.Mgunga na Meneja
Mradi wa FIT For the Fit Habiba Issa wameweza kutoa rai kwa wazazi na vijana
mbalimbali waewez kutumia fursa zinazo onekana hata kufikia malengo yao
waliweza kutoa mifano mbalimbali ambapo waliweza kuwataja wahitimu wallio
hitimu na kuweza kuwa waalimu na wengine kutoka nne ya nchi ikiwa ni idadi ya
zaidi ya wanafunzi 5 ambao waliweza kwenda nchini idia na nchi jirani,kwa
wazazi wawe na moyo wa kuwaleta watoto ili waweze kupata elimu ya sanaa
mbalimbali waache zana potofu ya kuwa sanaani uhuni usio kuwa na faida hayo
yamesemwa na viongozi hao wa mradi huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni