|
Na wao walibeba mabango yenye ujumbe huo |
|
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christine Ishengoma na Mratibu wa SPANEST, Godwell Olle Meing'ataki wakikagua timu ya Idodi FC |
|
Hapa wakikagua Kitisi FC |
|
Wakati timu hizo zikiingia uwanjani |
|
Kitisi FC wakionesha mabango yenye ujumbe Piga Vita Ujangili, Piga Mpira, Okoa Tembo |
|
Idodi FC wakiwa na mabango hayo |
|
Wasanii wakiimba wimbo unaohamasisha upigaji vita ujangili |
|
Nyomi ya watu |
|
Mkuu wa Mkoa akamaliza kwa kuzipa neno timu zinazoshiriki ligi hiyo kuxzingatia sheria za mpira |
|
Mbele ya kikombe kinachogombaniwa |
|
Vumbi uwanjani, hivi ndivyo ilivyokuwa |
|
Na waliofukuza kuku na kujinyakulia zawadi ya sh 30,000 walifanya hivi kwa upande wa wanawake |
|
Na kwa upande wa wanaume hali ilikuwa hivi
|
Hapa wakiwa katika mchezo wa kuvuta kamba
|
Kitisi waliibuka washindi |
|
|
NGUVU
za jitihada za SPANEST katika kulinda wanyama wa hifadhi ya Ruaha
Iringa na kupiga vita vitendo vya ujangili zimeanza kuonekana baada ya
kuja na mbinu mpya ya kuanzisha michuano ya soka kwa vijana
wanaozunguka hifadhi ya Taifa ya Ruaha .
Mratibu wa SPANEST, Godwell Olle Meing’ataki alisema
lengo la ligi hiyo yenye kauli mbiu “Piga Vita Ujangili Piga Mpira Okoa Tembo”
ni kuwaunganisha vijana katika vita dhidi ya ujangili wa wanyamapori wakiwemo
Tembo.
Alisema wazo la kuunganisha vijana katika
vita ya ujangili linaonekana kuwa njia muafaka ya kutokomeza ujangili kutokana
na ukweli kwamba vijana ndiyo walengwa wakubwa katika kushawishika kuingia
kwenye maeneo yaliyohifadhiwa na kufanya ujangili.
“Takwimu za ujangili katika maeneo
yaliyohifadhiwa zinaonesha kuwa vijana wengi hukamatwa katika matukio hayo.
Vijana hao hurubuniwa na watu wenye fedha ili wafanye ujangili,” alisema.
Akizindua michuano hiyo mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christine Ishengoma katika
mchezo uliozikutanisha timu ya Idodi FC
na Kitisi FC katika uwanja wa Shule ya Msingi Idodi.
Katika mashindano hayo wenyeji Idodi FC waliutumia vyema uwanja wao wa nyumbani na kufanikiwa kuibuka
vinara kwa kuichabanga Kitisi FC kwa mabao 2-0.
Bao la kwanza la Idodi FC lilipatikana Dk
23 ya mchezo kupitia kiungo wake mkabaji Same Gembe aliyopokea pasi safi kutoka
kwa mshambuliaji wao Maneno Fumbe na
kufanikiwa kupiga shuti kali lililomshinda golikipa wa Kitisi FC, Maneno
Ng’ingo.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Idodi
FC kuwa mbele kwa 1-0 bila dhidi ya Kitisi FC walioonekana wachovu muda wote wa
mchezo.
Katika kipindi cha pili cha mchezo, Idodi
FC waliongeza kasi na katika Dk 55 ya mchezo walifanikiwa kuongeza bao la pili
lililofungwa kupitia kiungo mshambuliaji, Amad Kambangwa.
Kuzamishwa kwa bao la pili kuliwafanya
wapinzani wao wapoteane zaidi na mpaka kipenga cha mwisho cha mchezo huo
kinapulizwa, Kitisi FC walikuwa wamelala kwa bao 2-0.
Mechi hiyo ilitanguliwa na mashindano mengine ya kufukuza kuku na kuvuta kamba kwa wawakilishi wa vijiji vya Idodi na Kitisi.
Akizindua mashindano hayo
yatakayozikutanisha timu 21 kutoka vijiji 21 vinavyozunguka hifadhi ya Taifa ya
Ruaha,
Kwa mujibu wa Mratibu wa SPANEST, mshindi
wa kwanza atapata kikombe, medali ya dhahabu, seti moja ya jezi, cheti, Sh
300,000, kutembelea Hifadhi ya Ruaha.
Mshindi wa pili atapata medali ya fedha,
mipira 2, cheti na Sh 200,000 taslim huku mshindi wa Tatu akipata medali ya
shaba, cheti na Sh 100,00 huku mshindi wa nne akipta Sh 50,000 katika ligi hiyo itakayomalizika Agosti 8, mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni