DIWANI  wa  chama   cha Tanzania
 Labour Party (TLP) kata ya  Lupingu  wilaya ya  Ludewa mkoani  Njombe  
John Kiowi amempongeza  mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe kwa
 jitihada zake   anazozifanya katika 
 kuwapelekea maendeleo wananchi wa Ludewa  huku akiwashangaa   wapinzani
 wanaopinga  jitihada  mbali mbali  zinazofanywa na serikali ya  chama  
cha Mapinduzi (CCM) na  kudai  kuwa  yeye  si mpinzani wa uchwara wa  
kupinga  maendeleo . 
  
Akizungumza  
 na  wanahabari  jana wakati wa  zoezi la mbunge  Filikunjombe  na  
diwani  huyo  kushiriki na  wananchi  wa kata ya 
 Lupingu  kuchimba mashimo ya nguzo  za umeme  na kusimika  nguzo hizo 
za umeme , Kiowi  alisema  kuwa   ni  zaidi ya  wabunge  watano  
wamepata  kuliongoza  jimbo  hilo la Ludewa  ila ni mara  yake ya 
kwanza  kuona mbunge akishiriki bega kwa  bega na wananchi wake  
kuchimba mashimo  kama ambavyo mbunge  huyo anafanya . 
  
"
 Jamani  wananchi  kwanza ni jambo la kumpongeza
 mbunge  wetu mbali ya kuhimiza wananchi ila mwenyewe  pia amekuwa 
mstali wa mbele katika  kushiriki tofauti na wana siasa  wengine ambao  
muda  wote  wao ni watu wa majukwaani ila  vitendo sifuri .....nasema  
Ludewa  imempata mbunge na niweke  wazi  hapa mimi  sio mpinzani hivi  
tujiulize wenyewe  nikisema mimi ni mpinzani napinga  nini hapa haya 
maendeleo  ni kwa  faida yangu na  wananchi  wote  sasa kama mbunge wa 
CCM wanafanya  kuna haja ya upinzani hapa " 
  
Kiowi 
 alisema kuwa ataendelea  kufanya kazi na mbunge  Filikunjombe ikiwa ni 
pamoja na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata  yake kwani 
chama  chake  cha TLP katika  kata ya Lupingu  kinatekeleza  ilani ya  
CCM ambacho  ndicho  chama  kilichopo madarakani na peke  yake  bila 
kumtegemea  mbunge hawezi  kufanya lolote. 
  
Diwani
 Kiowi ambae  alikuwa amevalia  sare  za CCM katika  shughuli  hiyo ya 
maendeleo  alisema kuwa  katika kuhakikisha kuwa yeye  si mpinzani ila 
ni mpenda maendeleo  hata  sare za CCM zinazotolewa na mbunge 
Filikunjombe amekuwa akizivaa na amekuwa mstali wa  mbele kumpongeza  
mbunge  huyo kutokana na kuwa mbunge wa mfano kwa kufanya kazi bila na 
makundi  yote . 
  
Hata  
 hivyo  diwani  huyo alisema kuwa katika  suala la maendeleo hata  kuwa 
tayari
 kuona  watu  wachache  wakimkwamisha mbunge  huyo kwa  kushindwa kuunga
 mkono jitihada  zake katika kuwaletea maendeleo na kudai kuwa  kwa  
upande  wake anaona  wapinzani ni  wana CCM wenyewe wasiopenda kujivunia
 maendeleo makubwa mbayo  mbunge  Filikunjombe ameyapeleka Ludewa . 
  
Kwa 
 upande wake  mbunge  Filikunjombe mbali ya kumpongeza diwani  huyo wa 
TLP kwa  kushiriki  vema katika  shughuli za maendeleo bado  alisema 
kuwa ni  wapinzani wachache
 nchini ambao  wanajitoa kama  diwani  huyo katika  shughuli za 
maendeleo  zinazoitishwa na mbunge wa CCM  
  
Alisema
 yapo  baadhi ya maeneo  wabunge ama madiwani wa upinzani  wamekuwa ni 
watu wa  kupinga kila jambo linalofanywa na mbunge ama diwani wa CCM  
na  wengine  wasiokuwa na uzalendo  na Taifa  wamefikia hatua ya kubeza 
hata jitihada zinazofanywa na Rais Dr Jakaya  Kikwete katika  kuliletea 
maendeleo  Taifa  jambo ambalo si la kizalendo hata kidogo na
 kuwa  huo si upinzani wa kweli. 
  
"
 Nataka  kusema  hivi wakati  wa kampeni ndio  wakati wa kupingana 
kisera ila baada ya chaguzi  hakuna  haja ya  kuendelea  kupingana ni 
kuwa  wamoja na kuwaletea  wananchi maendeleo hivi  hebu  niulize ujenzi
 huu wa barabara  ya Lupingu ,Ludewa  na Njombe Ludewa unaoendelea ni 
kwa  faida ya nani hii barabara  inatumiwa na wana CCM pekee  mbona  
hata  wapinzani mnapita katika barabara  hiyo  hiyo  sasa
 unapinga  nini wakati  huu wa CCM kutekeleza ilani  yake ....tuwe  na 
uzalendo  wa nchi  yetu tusiwe wa  kupinga kila  kitu na mimi nikueleze 
 wazi kama  ungejaribu kupinga mradi huu wa umeme  kwa  kutoshiriki 
tungeonana  wabaya mbele ya  safari" 
  
Akielezea 
 mradi huo wa umeme Filikunjombe  alisema kuwa kwa kasi  ambayo  
wananchi  wanaenda nayo katika  kujitolea  nguvu  zao kuchimba mashimo 
na  kusogeza nguzo katika mashimo  hayo ni 
 wazi  mradi huo wa umeme  utakamilika kabla ya  Desemba mwaka  huu . 
  
Aidha 
 alisema kuwa wakati akiingia madarakani mwaka 2010  ni  kijiji  kimoja 
pekee cha jimbo  hilo la Ludewa ambacho  kilikuwa na umeme  wa mafuta  
ila  sasa  zaidi  ya vijiji 10  vina umeme na kuwa hadi sasa   jumla ya 
 vijiji 49 vitafikiwa na mradi wa umeme huo ambao unatekelezwa kwa nguvu
 za  serikali ya Tanzania , Swedeni na kanisa na Romani Katoliki 
Dayosisi ya  Njombe. 
 | 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni