Na matukiodaimaBlogu.
WAKATI
maadhimisho ya siku ya mlipakodi nchini yameadhimisha leo nchini kote
mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa imekabidhi tuzo
mbili kwa a makampuni mawili yanayomilikiwa na familia ya kamanda wa UV
CCM mkoa wa Iringa Bw Salim Asas likiwemo kampuni la usafirishaji
mizigo la Asas Transporters Co. Ltd na ile ya usafilishaji wa
mafuta ya TransFuel Logistics Ltd baada ya kuongoza kwa ulipaji
mzuri wa kodi kwa mwaka 2013 /2014.
Akitangaza
washindi hao wakati wa maadhimisho ya siku ya mlipa kodi
yaliyofanyika kimkoa katika ukumbi wa IDYDC mjini Iringa meneja wa
mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa
Rosalia Mwenda alisema kuwa TRA imekuwa na utaratibu wa
kuadhimisha siku ya mlipa kodi nchini na kuwa kwa mkoa wa Iringa na
Njombe maadhimisho hayo yamefanyika katika mkoa wa Iringa kutokana na
mamlaka hiyo kuendelea kufanya kazi kama mkoa mmoja .
Alisema
kuwa kampuni hizo za Asas zimeweza kuongoza katika ulipaji kodi
katika kipengele cha mfanyabiashara mlipaji kodi mkubwa baada ya
makampuni mawili yanayosimamiwa na Asas moja kushika nafasi ya kwanza
ambalo ni lile kampuni ya usafirishaji ya Asas Transporters C.
Ltd kwa ulipaji kodi na nafasi ya pili ya walipaji kodi wa kati
pia imechukuliwa na kampuni ya usafirishaji mafuta ya Transfuel
Logistics Ltd ambayo pia ni sehemu ya makampuni ya shiriki ya Asas
Aliwataja
wengine walioongoza katika ulipaji kodi kuwa ni pamoja na MT Huel
Transporters , ambayo ilishika nafasi ya pili na nafasi ya tatu kwa
walipaji kodi wakubwa ni pamoja na Ruaha University College huku
upande wa walipaji kodi wa kati aliyeongoza na Iringa Foods and
Deverages Ltd nafasi ya pili Transfuel Logistics Ltd na nafasi ya tatu Kalenga West Parki Tours MOtel Ltd .
Wakati kwa wafanyabiashara wadogo
walioshinda tuzo hizo za vyeti maalum nafasi ya ya kwanza
alipewa BEder F. Kileo nafasi ya pili ilichukuliwa na Shakra Kiwanga
ambae ni mwenyekiti wa UWT wilaya ya Iringa na nafasi ya tatu
ilichukuliwa na Ahmed Tasha wakati kwa mshindi wa jumla kwa mkoa wa
Iringa na kanda ya nyanda za juu kusini akipewa tuzo hiyo Sao Hill
Forest Project .
Kwa
upande wa vituo vya radio kampuni ya Big Time Hinghland
co.Ltd(Radio Ebony Fm) nafasi ya pili kampuni ya Scope Tanzania Ltd (
Radio Countyr Fm) na nafasi ya tatu Qiblatain Fm Radio .
Wakati
kwa upande wa walipakodi bora wilayani kwa Mufindi ni SAo Hill
Forest Project iliyoshika nafasi ya kwanza na ya pili na ya tatu
kuchukuliwa na Chai Bora Ltd wakati wilaya ya Ludewa ni John Naoel
Haule ,nafasi ya pili ni Donata Linus MGaya huku nafasi ya tatu ni
Nathanael Mgaya , katika wilaya ya Makete aliyeongoza ni Felix
Eliud Sanga , Christopher s. Mahenge na nafasi ya Tatu ni
Shaibustolen Mahenge .
Wilaya
ya Njombe mshindi wa kwanza ni Philemon N . Mtewele nafasi ya
pili ni Augustino L . Kisinga na nafasi ya tatu kwa ulipaji kodi ni
Ndimi Enterprises Ltd .
Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo mkurugenzi wa kampuni za Asas
Bw Salim Abri asas ambae ni kamanda wa UV CCM mkoa wa Iringa alisem a
kuwa wajibu wa kampuni yake ni kuendelea kulipa kodi vizuri kama
sehemu ya kukuza uchumi wa Taifa na kuwa tuzo hizo ni heshima kwa
kampuni zake na kuwa ni chachu kwa wengine kupenda kulipa kodi .
Pia
alisema wapo ambao wanafikra tofauti kuwa ukiwa mwanasiasa ni mtu
wa kukwepa kodi na kuwa kampuni zake zipo kwa ajili ya kuona
uchumi wa Taifa unakua pamoja na kulipa kodi kwa wakati na kwa
mujibu wa taratibu za nchi .
Hata
hivyo alisema kuwa ukwepaji kodi hausaidii hata kidogo kwa ukuzaji
wa uchumi wa Taifa na kuwa kila mfanyabiashara anapaswa kuwa mzalendo
na Taifa lake kwa kulipa kodi badala ya kukwepa kulipa kodi .
"
Na mimi napenda kushukuru sana TRA kwa utaratibu huu wa kuwatambua
walipaji kodi wazuri na kuwapa vyeti hii ni heshima na changamoto
kubwa kwa wafanyabiashara wengine kulipa kodi vizuri "
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni