| Mwakilishi wa Continental Reliable Cleanring (T) Ltd and Fm Abri Bw Fahad Abri akiwa katika ukumbi huo | 
| Continental Reliable Cleanring (T) Ltd wakiwa katika ukumbi huo | 
KAMPUNI
 ya kizalendo ya  Continental Reliable Cleanring (T)   Ltd iliyopo  
chini ya kamapuni ya  Fm Abri na Famari Inverstment (T) Ltd  yenye 
makao  yake mjini Iringa na Dar es  
Salaam  imejipongeza  kwa  kufanikiwa  kuongoza nafasi ya  tatu katika 
mkoa  wa Dar e Salaam  kwa  ulipaji mzuri  wa  kodi nchini. 
Akizungumza  mara 
 baada ya  kukabidhiwa   cheti hicho jana katika  maadhimisho ya  siku 
ya mlipa  kodi yaliyofanyika kitaifa  katika Ukumbi wa  Mikutano wa 
Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam  mkurugenzi 
mtendaji  wa kampuni hiyo Bw Abbdalallah Abri  alisema  kuwa kampuni  
yake  inajivunia kwa  kushika  nafasi ya  tatu kwa mkoa  wa Dar es 
Salaam  kwa  ulipaji mzuri wa  kodi. 
Hapa 
 hivyo  alisema mafanikio hayo  yanaiwezesha kampuni  hiyo  kuendelea  
kujenga  heshima  kubwa katika Taifa ila  pia  kuongeza  ufanisi  zaidi 
 wa utendaji kazi  wake na hali ya uaminifu ambayo  ndio msingi mkubwa 
kwa maendeleo ya Taifa . 
Abri 
 alisema  kuwa  ili  Taifa   kuendelea  kujenga uchimi imara   ni  
wajibu  wa kila mfanyabiashara   kuonyesha  uzalendo wake  kwa  kulipa  
kodi na kuwa   wao kama wamiliki  wa kampuni ya  kizalendo ya Continental
 Reliable Cleanring (T)  Ltd iliyopo chini ya kamapuni ya  Fm Abri  na Famari Inverstment (T) Ltd 
kamwe  hawatakuwa  nyuma katika ulipaji  kodi  nchini. 
"
 Kweli  tunajivunia nafasi hii ambayo tumeishika kuwa nafasi ya tatu 
kwa  mkoa kama Dar es Salaam ambao  una makampuni  mengi zaidi na  
wafanyabiashara wengi  wakubwa ni jambo la  kujivunia sana " 
Hata 
 hivyo  alisema  kuwa  ushindi  ambao kampuni hiyo  imeupata  wa  
ulipaji kodi  ni heshima  pia  kwa  wateja  wake ambao  wameendelea  
kujenga imani na kampuni  hiyo kwa kuendelea  kuitumia katika uagizaji  
mizigo mbali mbali yakiwemo magari na  kuwa heshima hiyo itaendelea  
kujengwa  zaidi na makampuni   yote yaliyopo chini ya Continental 
Reliable Cleanring (T)  Ltd  na mengine  yanayomilikiwa na Fm Abri . 
 | 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni