  | 
| Bi  Sarah Mungai akiwa na mmoja kati ya  watoto yatima wa kituo cha DBL mkimbizi Iringa  | 
  | 
| Bi  sarah Mungai akiwa na Mtoto  aliyetupwa na  mama  yake  mzazi ambae anautindia  wa  ubongo  mara  baada ya  kumzaa na sasa anaendelea vema baada ya  kuokolewa maisha yake  na kituo cha DBL Iringa  | 
  | 
| Mkurugenzi wa kituo  cha DBL Neema Mpeli  kulia akiwa na sarah Mungai  | 
  | 
| Mkurugenzi mtendaji wa DBL mchungaji Mpeli  Mwaisumbi akimkaribisha  Mungai na mkewe  | 
  | 
| Baadhi ya  watoto  kituoni hapo  | 
  | 
| Mchungaji Mpeli  akieleza jinsi ambavyo Mungai alivyokuwa msaada  kituoni hapo  | 
  | 
| Bi.Sarah Mungai  akisoma  risala ya familia  | 
  | 
| Mchuungaji Mpeli  akiwashukuru wadau  | 
  | 
| Watoto yatima  wakifurahia msaada   huo  | 
  | 
| wageni  mbali mbali  waliofika katika  hafla   hiyo  | 
  | 
| Sarah Mungai na Mumewe  Geofrey wakitoa taarifa  yao fupi  | 
  | 
| Mmoja wa watoto yatima  akishukuru  | 
  | 
| Geofrey na mkewe  wakiwaongoza  yatima  kupata chakula  | 
  | 
| Mtoto aliyetupwa  | 
  | 
| Dr Gabone  akishiriki  chakula  | 
  | 
| Mungai akimlisha chakula  yatima  | 
  | 
 Na matukiodaimablog
MKANDARASI 
 Geofrey  Mungai  ametoa  msaada  wa  nguo za sikukuu na chakula vyote  vikiwa na  thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2  wa kituo cha  watoto yatima cha  Daily Bread Life Tanzania  (DBL) kwa ajili ya  kusherekea sikukuu ya krismass na mwaka mpya.
Mungai
 alitoa  msaada huo jana  kwa  uongozi  wa  kituo hicho pamoja na 
kuwaandalia chakula  cha pamoja   watoto  zaidi   39  na  wananchi mbali 
mbali wa mji  wa Iringa kama njia ya  kuwahamasisha  kusaidia yatima .
Akizungumza 
 kwa niaba ya familia ya Mungai mke wa mkandarasi huyo Sarah Mungai   alisema  kuwa imekuwa ni
 kawaida  yake  kwa  kila mwaka katika msimu  wa  sikukuu ya Krismas na 
mwaka  mpya  kufika katika  kituo hicho na  kuwapa msaada  watoto  hao  
ili nao  kuungana na  watoto  wenye  wazazi  wao kufurahia sikukuu hizo.
Hata 
 hivyo  alisema  kuwa jamii ya  mkoa  wa Iringa na  watanzania  kwa 
ujumla wanapaswa  kubadilika kwa  kuelekeza  michango  yao  kwa  watoto 
 yatima ambao baada ya  kupoteza  wazazi  wao  faraja ya  pekee  
wanaisubiri  kutoka kwa  jamii inayowazunguka.
Aidha 
 alisema  kuwa  yeye  kama mmoja kati  ya wananchi wa Iringa wenye mapenzi mema na watoto yatima hivyo kuwaomba wananchi wengine   kuweka  mpango wa  
kuendelea  kutembelea  vituo  vya yatima kila mwaka  kwa  ajili  ya 
kuwasaidia misaada  mbali mbali.
  
Alisema 
 kuwa  upo uwezekano mkubwa wa  watoto  hao yatima  kuendelea   
kusaidia  iwapo watanzania na wadau  mbali mbali   kuwekeza kwa  watoto hao.
Kwa 
 upande  wake  mkurugenzi mtendaji  wa  kituo  hicho  mchungaji Mpeli 
Mwaisumbi mbali ya  kumpongeza  Mungai kwa  kuendelea  kusaidia  watoto 
 hao  bado wadau  mbali mbali  wameendelea kujitolea kusaidia  kituo hicho .
"watoto  hao wanalilewa  vema na  wapo ambao  wanasoma shule  mbali mbali   na  vyuo  vikuu baada ya kusaidiwa na  wadau"
 Alisema 
 kuwa  kituo  hicho kinafanya kazi  chini  ya  shirika  lisilo la 
kiserikali  ya Daily Bread  Life  Tanzania lililosajiliwa  kwa  usajili 
 12903 chini ya  wizara ya mambo ya ndani ya  nchi pia   kituo  
kimesajiliwa na ustawi  wa jamii kwa  kupewa usajili wa makao  ya  
watoto namba 00049995.
Hata 
 hivyo  alisema  kuwa  kituo  kilianza  kupokea  watoto  14 mwaka  2004 
na  sasa  kuna  watoto 37 waliopo  kituoni  hapo  na  kuwa  toka  kituo 
 kianzishwe  jumla  ya  watoto 51 wamelelewa  hapo 
Alisema 
 kutokana na misaada wa  wadau mbali mbali kituo kimeendelea  kupata  
mafanikio makubwa kama  kuwa na  shamba  ,basi  moja ,mradi  wa 
cherehani pia  tayari   shule  ya  sekondari 
ya DBL imejengwa na imeanza  kupokea wanafunzi toka mwaka huu  shule  iliyopo  umbali  wa kilomita 6  kutoka mjini Iringa kwa  lengo 
kuwawezesha  watoto  na wengine  watyakaofaulu na kukosa nafasi  kupata  elimu ya  sekondari.
Pia 
 alisema changamoto  kubwa katika 
 uendeshaji wa  kituo hicho ni michango mingi katika shule za msingi 
ambako  watoto  hao  wanasoma ,kukosa  ruzuku toka  serikalini na  
changamoto  nyingine  nyingi.
Mchungaji
 Mpeli  aliwaomba  watanzania  na  wadau mbali mbali pale  walipo  
iwapo  wanahitaji kusaidia  kituo hicho  kutuma  michango  yao kupitia 
akaunti namba Benk ya Exim ni 5435526007  Daily Bread  Life Childreans home ,ama  kwa njia ya M-PESA  0754362536
MWISHO
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni