HOPE SERVICE STATION

nsekwa

ALTEZA

Jumamosi, 24 Mei 2014

MBARONI KWA KUINGIA NCHINI KWA NJIA ZA PANYA

Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia watuhumiwa wawili Raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia Nchini bila kibali.
 
Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake Kamanda wa polisi Mkoani hapa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 20 mei majira ya saa 4 Asubuhi huko maeneo ya barabara mbili iliyopo kata ya Makorongoni.
 
Kamanda aliwataja watuhumiwa hao ni Saimoni Bolisha (22) pamoja na Maraku Thadesa na kusema watu hao walikamatwa wakati askari wakiwa doria maeneo hayo.
 
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni