HOPE SERVICE STATION

nsekwa

ALTEZA

Jumatano, 28 Mei 2014

HIVI NI KWELI DAUDI BALALI ALIKUFA ?

  

 Mdogo  wake wa aliyekuwa gavana wa benki kuu Tanzania Daud Balali  Bw Pachal Balali akiwa kando ya makaburi  ambayo familia  huwa inazikana eneo la Luganga Mafinga
Marehemu Daudi Balali

pemeibuka maswali zaidi ya majibu kuhusu ‘kutoweka’ kwa aliyekuwa gavana wa benki kuu Dr. Daudi Balali. Maswali mengi yanaibuka kufuatia kuwepo kwa akaunti ya twitter inayodaiwa kuwa ni ya Balali na ambayo hutoa post na picha zinazoashiria kuwa mwenye akaunti hiyo yupo:

Nitajie nchi yeyote zaidi ya Tanzania ambayo Gavana wake wa Benki Kuu aliugua na kufa na hakuna hata picha moja ya mazishi yake kwa umma.

Michuzi alisema haya kunako Agosti 2008:
Mwili wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dr. Daud Timoth Said Ballali (65) aliyefariki Ijumaa iliyopita umehifadhiwa katika Nyumba ya Maziko ya De Vol iliyoko mjini Washington DC, nchini Marekani ambako inasubiri mazishi siku ya Ijumaa.


Taratibu za ibada na mazishi ambazo KLHN imepata nafasi ya kuziona inaonesha kuwa Gavana Balali alifariki tarehe 16 hapo Washington DC na atazikwa hapo hapo siku ya Ijumaa. Misa ya kumwombea Marehemu itafanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Stephen Shahidi mjini Washington DC anuani yake ni ST. STEPHEN MARTYR CHURCH 2436 Pennsylvania Ave, NW Washington, DC 20037.

Ibada hiyo ya mazishi itaenda sambamba na kuuona mwili wa Marehemu kuanzia saa nne asubuhi. Hata hivyo shughuli hiyo nzima ni kwa ndugu, jamaa, na marafiki wa karibu na si kwa hadhara ya kila mtu atakaye kushiriki. Marehemu atalazwa katika makaburi ya Wakatoliki ya Gate of Heaven eneo la Silver Spring, MD.

 
Hata hivyo haijajulikana kwa uhakika kama mwili wa marehemu utazikwa ardhini kama ilivyo desturi ya kiafrika au utateketezwa kwa moto kwani makaburi hayo yanatoa huduma hiyo pia. Kama ulikuwa ni usia wake kuteketezwa basi kwa kanuni za Kanisa Katoliki basi itafanyika mara tu baada ya ibada.


 Kwa kanuni za Kanisa Katoliki mwili uliolazwa kwa njia ya kuteketezwa kwa moto mabaki yake (majivu) hawapewi familia, kusambazwa au kugawanywa katika mafungu madogomadogo na badala yake ni lazima viwekwe ardhini au kwenye sehemu maalumu inayotumika kwa maziko ya namna hiyo.

Dr. Balali ambaye amefariki akiwa amezungukwa na wingu kubwa la kashfa dhidi yake na dhidi ya taasisi aliyoingoza inasemakana aliacha usia uliotaka atakapofariki basi azikwe Marekani. 


Hata hivyo pamoja na kashfa nyingi zilizoandikwa na vyombo mbalimbali vya magazeti na kutangazwa majukwaani Bw. Balali hakuwa mtuhumiwa yeyote na hakukuwa na kesi yoyote ile ya kihalifu dhidi yake na hivyo amekufa kama raia na mtu huru.

Hata hivyo Dr. Balali ilidaiwa kuwa aliandika barua ya kutaka kujiuzulu kutokana na hali mbaya ya kiafya uamuzi ambao 


haukujibiwa hadi pale taarifa ya uchunguzi wa EPA ilipotoka na Rais Kikwete kutengua uteuzi wake kama Gavana wa Benki Kuu. 


Hata hivyo, taarifa ya Rais iliyosomwa na Katibu Mkuu kiongozi haikusema kama Gov. Ballali ni mhalifu, anatafutwa, au kwa namna yoyote ile amefanya makosa ya kisheria. 

Hilo lilithibitishwa siku chache zilizopita ambapo Ikulu walitangaza kuwa walikuwa hawamtafuti Ballali na ya kuwa kokote alikokuweko alikuwa ni “mtu huru”.

Ni kwa sababu hiyo basi ibada ya mazishi inatarajiwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiongozwa na Balozi wa Tanzani nchini Marekani Bw. Ombeni Sefue, watumishi wa idara mbalimbali alizowahi kuzitumikia ikiwemo IMF, ndugu zake ambao wamewasili siku chache zilizopita, na baadhi ya Watanzania kadhaa waishio maeneo ya Washington DC.


Gavana Ballali ameacha mke na familia.
Raha ya milele umpe ee Bwana
Na mwanga wa milele umuangazie
Apumzike kwa amani.

Amina.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni