Mwili wa Marehemu Munuo ukitolewa katika Gesti hiyo
Mwili wa Marehemu Munuo ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama
Mtumishi
wa idara ya Afya katika halmashauri ya mji wa kahama, Mkoani Shinyanga,
Jeremiah Munuo (50) amekutwa amefariki dunia katika nyumba moja ya
kulala wageni mjini Kahama.
Taarifa
kutoka jeshi la polisi wilayani humo zimesema kwamba Tukio hilo
limetokea usiku wa kuamkia leo katika nyumba hiyo iitwayo KK Lodge
iliyopo jirani na ofisi za Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Taarifa
zimesema watumishi wenzake walikwenda kumuona leo majira ya saa 6
mchana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa kwa muda mrefu.
Jeshi
la polisi wilayani Kahama limefika katika eneo la tukio na kumkuta
marehemu Munuo ambaye alikuwa na miezi 3 tu tangu ahamishiwe katika
halmashauri hiyo akiwa na Fedha taslimu shilingi 596,000 na simu nne za
mkononi.
Mwili
wa marehemu Munuo umepelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia
maiti cha hospitali ya wilaya hiyo na uchunguzi juu ya tukio hilo bado
unaendelea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni