MWENYEKITI WA BARAZA LA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI NCHINI (NACOPHA) BWANA VITALIS MAKAYULA.
Imeelezwa
kuwa kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi katika maeneo ya mijini ni kubwa
kuliko maeneo ya vijijini hali inayosababishwa na mwingiliano wa watu na
shughuli za kiuchumi.
Hayo
yameelezwa leo jijini Mwanza na mwenyekiti wa baraza la watu wanaoishi na
virusi vya ukimwi nchini Vitalis Makayula katika warsha ya siku tatu ya watu
wanaoishi na virusi vya ukimwi iliyoandaliwa na shirika la AGPAHI.
Makayula
amesema kuwa kwa sasa maeneo ya mjini kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi
ni asilimia 7.2 tofauti na vijijini ambayo ni asilimia 4.3.
Akielezea
mikoa yenye maambukizi makubwa Makayula ameitaja kuwa ni pamoja na Njombe yenye
asilimia 14.8,Iringa asilimia 9.1 na Mbeya yenyeasilimia 9.0.
AFISA MRADI KUTOKA SHIRIKA LA AGPAHI BI CECILIA YONA AKIWA NA MR ATUGONZA KUTOKA JIJINI DAR ES SALAAM.
Akitoa
malengo ya warsha hiyo Afisa mradi wa mpango wa watu wanaoishi na virusi vya
ukimwi kutoka shirika la AGPAHI Bi Cecilia Yona amesema ni kupata uelewa wa
shughuli za hospitali za rufaa pamoja na kushiriki mipango ya shughuli za
ukimwi katika ngazi za vijiji hadi wilaya.
Awali
akifungua warsha hiyo Meneja wa mradi kutoka shirika la AGPAHI Shinyanga
Dr.Gastor Njau amesema kuwa warsha hiyo ni muendelezo wa kuwapa elimu WAVIU ili
kuendelea kusaidia kutoa huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni