Rai hiyo imetolewa jana na Katibu mkuu wa mkoa wa vyuo vikuu
vya Chama cha mapinduzi, Christopher Ngubiagai, alipokuwa akitunuku
vyeti kwa viongozi waliomaliza muda wao miaka mitatu kutoka vyuo vikuu
vya Arusha na Tumaini (Makumira) kwenye mahafali ya wanachuo hao wa
mwaka wa tatu hafla iliyofanyika chuo kikuu cha Arusha.
Aliwaambia wahitimu hao wa mwaka
wa tatu katika vyuo hivyo kuwa wasiridhike na kiwango cha elimu
waliyoipata bali waongeze bidii kwa kuwa vyuoni ni mwanzo tu wakupata
mafanikio katika maisha.wajiendeleze zaidi ili kuhimili soko la
ushindani la kielimu katika nchi za Afrika mashariki na mataifa mengine
Ulimwenguni.
Ngubiagai, ambae pia ni mjumbe
wa halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi,(NEC) alisema kuwa kipindi
kilichopo sasa ni kwa wasomi hao kutambua kuwa ajira kwa sasa hazipo na
zinazopatikana hazitoshelezi mahitaji hivyo ni lazima wajiandalie
mazingira ya kujiajiri na si vinginevyo.
Alisema ni bora wasomi
wakalitambua hilo mapema wataweza kuondokana na mawazo na fikra za
kuajiriwa ambazo hazipo bali fursa iliyopo ni kujiajiri na wasisome kwa
matarajio ya kuajiriwa ndani ya serekali au sekta binafsi.
‘’Ndugu zangu ninataka niwaeleze
ukweli kwamba ajira zinazopatikana hazitoshelezi hivyo kikubwa ni ninyi
wasomi wa vyuo vikuu kusoma Kwa kujijengea mazingira ya kujiajiri na
mafanikio yatapatikama.’’alisema ngubiagai.
Na kamwe wala wasitarajie
kupata ajira kwa urahisi kutokana na ongezeko la wasomi wanaohitimu vyuo
vikuu kila mwaka hapa nchini.
Aliwaambia wanavyuo hao kuwa
Chama cha mapinduzi kimerejesha matawi ya Chama kwenye vyuo vikuu ili
kufundisha, itikadi ,malengo, ilani, Katiba ya CCM,elimu ya kujitegemea
na uzalendo .
Ngubiagai, aliwaambia wasomi hao
kuwa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi katika kurejesha matawi hayo
imepitisha kanuni ambapo kutakuwa na katibu mtendaji wa mkoa wa vyuo
vikuu,wajumbe4 watano wa NEC, na wasomi watatu ,ambao wote watakuwa ni
wajumbe wa NEC.
Kuhusu mikopo inayotolewa na
bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, Ngubiagai, amewaambia kuwa
haitoshelezi kutokana na ongezeko la vyuo vikuu nchini hivyo wasomi
hawana budi kukaa pamoja na kutafuta ufumbuzi ili mikopo iweze
kutosheleza mahitaji.
Akifafanua tuhuma zinazotolewa
na vyama vya kisiasa kuhusu ziara ya Katibu mkuu wa CCM, Komredi,
Abdulahaman Kinana, kuandamana na mawqaziri , watendaji wa serikali na
halmashauri kwenye ziara zinazofanywa na katibu mkuu huyo.
Ngubiagai, alisema kuwa Kinana
ndie katibu mkuu wa CCM, anakagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani
ya uchaguzi iliyoiweka na serikali ya CCM, madarakani, Ilani ambao ni
mkataba kati ya wananchi na serikali yao.
Pia ziara hiyo inapokea na
kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi ndio maana Katibu mkuu
huyo anaambatana na mawaziri, au watendaji wa serikali na halmashauri
ili kufafanua kero na kutoa majawabu sahihi .
Awali mwenyekiti wa tawi la chuo
kikuu cha Arusha, Daniel Limbu, alisema kuwa tawi hilo lilianza mwaka
2007 likiwa na wanachama 50 ,kutokana na chamgamoto zilizxojitokeza
kipindi kilichopita, hivi sasa tawi lina wanachama zaidi ya 250 amao
wote ni wanavyuo vikuu vya Arusha na Tumaini.
Alisema kuwa katika mahafali hayo wanachama 80 kutoka katika vyuo hivyo wamehitimu masomo yao vyuoni hapo,
Aliongeza kuwa vyuo hivyo pia vimepokea wanachama wapya zaidi ya 50 ambao ni wanavyuo mbali mbali hapa mkoan
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni