Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Rechel Kissanda kulia akitoa kauli ya kukataa kuzindua jengo hilo mbele ya mbunge Deo Filikunjombe kulia |
KIongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa akionyesha nyufa katika jengo hilo jipya huku msimamizi mkuu akitazama kulia |
Hapa akisisitiza usimamizi mzuri wa miradi ya umma |
Hapa kiongozi huyo akimuuliza juu ya nini kifanyike katika jengo hilo |
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa kushoto akikabidhi vyandarua kwa wanawake wajawazito katika kituo cha Manda wilaya ya Ludewa |
Hatua ya kiongozi huyo kukataa kuzindua jengo hilo iliungwa mkono na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ambae pia alisema anaungana na kiongozi huyo wa mbio za mwenge katika kupinga ujenzi huo uliofanyika chini ya kiwango .
Viongozi hao walifikia hatua hiyo juzi wakati wa uzinduzi wa jengo hilo kupitia mbio mbio hizo za mwenge wa Uhuru kwa kauli moja viongozi hao walisema kuwa hatua ya jengo hilo kuanza kuonyesha nyufa ni wazi kuwa mkandarasi aliyepewa kujenga jengo hilo ameifanya chini ya kiwango huku mganga mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa akiendelea kumtazama bila kumchukulia hatua .
Hivyo kiongozi huyo wa mbio za mwenge alisema kwa maelezo waliyoyapata kwa viongozi wa kitaifa akiwemo Rais Dr Jakaya Kikwete ni kutokubali kufungua majengo ama miradi iliyojengwa chini ya kiwango ili kulinda uharibifu wa fedha za umma.
"Ndugu zangu viongozi na mganga mkuu wa wilaya ya Ludewa umeziona nyufa hizi katika jengo lake sasa hili jengo hata kutumika bado ila linaonyesha nyufa ...sikia sipo tayari kuzindua jengo hili hadi mtakapolifanyia marekebisho ...:" alisema kiongozi huyo
Mbali ya mganga mkuu huyo kuahidi kulifanyia marekebisho bado kiongozi huyo alionyesha kuhoji fedha za kulifanyia marekebisho jengo hilo zitatoka katika mfuko gani.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Bw Filikunjombe pia aliungana na kiongozi huyo kuingiwa na shaka juu ya ujenzi huo na kudai kuwa anaungana na kiongozi huyo katika kupinga ujenzi huo.
"Mheshimiwa kiongozi wa mbio za mwnge nami naungana nawe katika hili mimi nipo na wewe kwani macho na masikio ya hawa wananchi ni kwetu viongozi iwapo tutakubali ujenzi kama huu ni hatari kwa wananchi wetu "
Hata hivyo mbali ya kulikataa jengo hilo bado kingozi huyo wa mbio za mwenge wa Uhuru baada ya kutoka nje ya jengo hilo aliweza kulizindua kwa shingo upande huku akisisitiza umakini wa watendaji katika kusimamia miradi ya umma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni