Mwanamuziki na kiongozi wa bendi ya Mapacha watatu Kahalid
chokoraa anategemea kupanda ulingoni jumamosi ya tarehe 24 katika ukumbi wa
friends corner kuzipiga na bondia
chipukizi mwenye uchu wa ushindi muda
wote awpo ulingoni Abdul manyenza. Chokoraa alisema muda mrefu amekuwa akifanya
mazoezi ya kujenga mwili na ya ngumi kwa
muda mrefu na amekuwa akipigana na mabondia tofautitofauti mazoezini na kuona
uwezo wao ni wa kawaida, hivyo anataka
kuwaonesha kama ana kipaji kingine zaidi ya kuimbia, kwa sasa amekuwa
akijifua katika gym ya bigright boxing ya mwananyamala chini ya mwalimu wake bondia mkongwe omar athuman ‘van dame’ kwa lengo la
kumsambaratisha mpinzani wake ambae amekuwa akijitapa kumfukuza chokoraaa kwa
kipondo kikali arudi kuimba. Siku hiyo ya jumamosi kutakuwa na mapambano ya
ubingwa kati ya Karama nyilawila na Said Mbelwa
wakigombea ubingwa wa UBO-AFRICA
,wakisindikizwa na kina chokoraa na
Abdul manyenza, Suleiman Galile akimkabili Abdala Pazi ‘kiroba’ nae bingwa wa afrika Alan kamote wataoneshana
umwamba na Adam ngange, Ramadhan kumbele atazipiga na Hassan kiwale”morobest” ,
idd athuman na julias kisarawe, nao wababe wa majigambo Zumba kukwe
wataoneshana kazi na Kamanda wa makamanda, pia kutakuwa na pambano mengine
mengi tu ya utangulizi ya mabondia wa tanga watazipiga na mabondia wa dare es salaam.
Kama vile Athuman boxa wa tanga atazipiga na waite juma wa chalinze, Rajabu
mahoja wa tanga atazipiga na kaisi wa darn a mengineyo yenye kuleta hamasa na
burudani za mchezo wa ngumi, kwa vijana kuonesha vipaji vyao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni