AMINI kila kukicha na mambo
mapya yanaibuka hii kwa mkoa wa Iringa ilikuwa ni vigumu sana kusikia
mwanamke akilazimisha kulipwa chake ila sasa imeanza baada ya
mwanamke mmoja ambae amekuwa akifanya biashara ya kuuza mwili wake
(Changudoa) kusafisha nyumba ya mfanyabiashara huyo jina linaanza na
herufi S baada ya kushindwa kumlipa chake.
Tukio
hilo limetokea asubuhi ya leo eneo la Ilala mjini Iringa baada ya
mwanaume huyo kumwacha mwanamke huyo ndani ya chumba chake kwa
kisingizio cha kwenda kumnunulia supu bila kutokea hadi mida ya saa 5
asubuhi .
Mpashaji
wetu amesema kuwa mfanyabiashara huyo amekuwa na kawaida ya kuingia na
wanawake tofauti tofauti ndani ya chumba chake na kulala nao hadi
asubuhi na jana kama kawaida yake aliingia na mwanamke huyo .
Hata
hivyo alisema baada ya kutoka asubuhi wao kama majirani walijua
amekwenda katika shughuli yake ya kuuza duka na ndani ya chumba chake
hakuna mtu baada ya kuufunga mlango huo kwa nje .
Katika
Hali ya kushangaza ni pale kijana mmoja ambae ni rafiki wa
mfanyabiashara huyo kufika na kumfungulia mlango mwanamke huyo ili
atoke nje.
Alisema
kutokana na mfanyabiashara huyo kushindwa kumpa ujira wake wa Tsh
50,000 kama walivyopatana mwanamke huyo aliamua kuchukua Sabufa na
kutokana nayo huku akitaka kumpa kichapo kijana huyo.
Mwanamke huyo amesema amelazimika kuchukua Sabufa hiyo ili kufidia deni ambalo anamdai mwanaume huyo.
Uchunguzi
wa mtandao huu umebaini kuwa mwanaume huyo hana mke baada ya kutengana
nae na ndio sababu ya kuendekeza michepuko kama hiyo |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni